Pata taarifa kuu

Kandanda: Nambari 2 wa FIFA Fatma Samoura kuondoka mwishoni mwa mwaka huu

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, Fatma Samoura, mwanamke wa kwanza na wa kwanza asiye Mzungu kuwa nambari 2 katika shirikisho la kandanda duniani mwaka 2016, ataacha wadhifa wake mwishoni mwa mwaka huu ili kutumia "muda zaidi kwa familia yake", FIFA imetangaza siku ya Jumatano Juni 14, 2023.

Msenegali Fatma Samba Diouf Samoura aliteuliwa Mei 2016 na bodi ya FIFA kuwa katibu mkuu washirikisho hili la Soka Duniani.
Msenegali Fatma Samba Diouf Samoura aliteuliwa Mei 2016 na bodi ya FIFA kuwa katibu mkuu washirikisho hili la Soka Duniani. Fifa
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuhudumu katika Umoja wa Mataifa, Msenegali huyo mwenye umri wa miaka 60 aliteuliwa Mei 2016 kufuatia kuchaguliwa kwa Mtaliano wa Uswisi Gianni Infantino kama rais wa shirika hilo, na kusaidia "kurudisha uaminifu wake" baada ya kashfa kadhaa, FIFA imeongeza katika taarifa kwa vyombo vya habari.

"Soka la wanawake litakuwa limefikia kilele kipya chini ya uongozi wake", limebaini shirika hilo, wakati kuchezwa kwa michuano ya Kombe la Dunia ya Wanawake nchini Australia na New Zealand (Julai 20-Agosti 20) ndio lengo kuu la mwisho la kiongozi huyo.

Fatma Samoura amechagua kukatisha "uvumi kuhusu nafasi (yake)" kwa kutarajia tangazo la kujiuzulu, ambalo alipanga kurasimisha "wiki ijayo" na Baraza la FIFA, akielezea kwamba alitaka kujitolea kwa familia yake mwaka ujao.

FIFA haikuonyesha dalili zozote za mtu atakaye chukua nafasi yake, wakati N°2 alionekana kwa kipindi cha miaka saba kama ya muelewa na mtu mwenye busara kama vile Gianni Infantino alivyokuwa mkali na mwenye migawanyiko, na kuzidisha mapendekezo ya mageuzi - wakati mwingine ambayo hayajakamilika, kama vile kupitishwa kwa michuano ya Kombe la Dunia ya kila miaka miwili - na kauli zenye utata.

"Kujiunga na FIFA ulikuwa uamuzi bora zaidi ambao nimefanya maishani mwangu. Nina furaha kuongoza timu tofauti," amesema Msenegali huyo, aliyeteuliwa bila uzoefu wa michezo lakini kwa kazi ndefu ya mwanadiplomasia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.