Pata taarifa kuu

Kundi B: Marekani na Wales zatoka sare kwa kufungana (1-1)

Bao pekee la Marekani limefungwa na Timothy Weah, mtoto wa George Weah, nyota wa zamani wa soka na rais wa sasa wa Liberia.

Timothy Weah (katikati), akivaa namba 21 mgongoni akisherehekea bao lake dhidi ya Wales.
Timothy Weah (katikati), akivaa namba 21 mgongoni akisherehekea bao lake dhidi ya Wales. © AFP - ANNE-CHRISTINE POUJOULAT
Matangazo ya kibiashara

Marekani na Wales zimetoka sare ya 1-1 siku ya Jumatatu kwa mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia, na kuchukuwa na fasi ya kufuzu katika kundi ambalo Uingereza imeibwagiza Iran 6-2.

Kupindi cha kwanza kila upande: sawa na vile "Team USA", timu ya taifa ya Marekani iliongoza 1-0 hadi mapumziko, kwa goli lake lililofungwa na Timothy Weah  katika dakika 36 ya mchezo, baada ya kuwakosesha amani Wales kwa kipindi cha dakika 45, sawa na "Dragons" ambao walifunga bao lao la kusawazisha lililopachikwa wavuni na Gareth Bale katika dakika ya  82 ya mchezo kwa mkwaju wa penalti), baada ya kipindi cha pili ambapo walitumia nguvu nyingi na utashi.

Wales ambao Wanashiriki tena michuano ya Kombe la Dunia baada ya kukosekana kwa miaka 64, waliungwa mkono na kundi la mashabiki wenye shauku na waliovalia mavazi mekundu.

Lakini tangu mwanzo wa mchezio, Marekani, ambayo ina wanawashezaji vijana zaidi katika mashindano (baada ya Ghana), walitawala mchezo dhidi ya  Waingereza, na kuchukua udhibiti kamili wa safu ya kati.

Nafasi ya kwanza ya wazi ilikuja dakika 10 tu kabla ya mchezo, wakati Josh Sargent alipoweka mpira wa kichwa wenye nguvu kwenye lango.

Ilifikiriwa basi kwamba Dragons itaangushwa haraka. Lakini wachezaji wa Rob Page, walishindwa kuendeleza soka lao, walikuwa katika nafasi nzuri ya ulinzi. Na hatimaye kwenye nafasi yao ya pili pekee ambapo "Team USA" ilifungua ukurasa wa mabao.

Timothy Weah, mtoto wa Rais wa Liberia

George, babake, aling’ara akiwa na Paris au AC Milan kabla ya kuwa rais wa nchi yake, Liberia. Lakini  Timothy, mtoto wa kiume wa George Weah, ambaye alipandisha jina la familia yake katika Kitabu cha Dhahabu cha Kombe la Dunia, akifungua bao la Marekani.

Vijana hawa wote wa Marekani wanapata uzoefu huko Qatar ambao, wanatumai, itakuwa muhimu kwao katika miaka minne ijayo, kwa michuano ya Kombe lao la Dunia nyumbani mnamo 2026, ambapo Marekani itaiandaa kwa pamoja na Canada na Mexico).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.