Misri yajiunga na timu nyingine tano ambazo zinaingia katika 16 bora ya AFCON
Bingwa mara saba wa taji la soka kwa mataifa ya Afrika Misri, imefuzu katika hatua ya 16 bora, kutafuta ubingwa wa mwaka huu, baada ya kuishinda jirani zao Sudan bao 1-0 katika mechi yake ya mwisho ya kundi D.
Imechapishwa:
Timu nyingine katika kundi hili Nigeria, imemaliza katika nafasi ya kwanza katika kundi hilo kwa alama 9 na kufuzu baada ya kuifunga Bissau 2-0.
Mataifa mengine yaliyofuzu katika hatua ya 16 ni pamoja na wenyeji Cameroon, Burkina Faso, Gabon, Senegal, Cape Verde, Guinea, Morocco na Malawi.
Ratiba ya timu zitakazofuzu zinatarajiwa kufahamika Alhamisi usiku, baada ya mechi za mwisho.
Kundi E
Cote Dvoire vs Algeria
Sierra Leon vs Equitorial Guinea
Kundi F
Gambia vs Tunisia
Mali vs Mauritania
Katika hatua nyingine, wachezaji 12 kati ya 28 wa Tunisia, wameambukizwa virusi vya Corona, kuelekea mechi yao ya mwisho ya kundi F dhidi ya Gambia siku ya Alhamisi usiku.
Hatua hiyo imeiacha Tunisia na wacheaji 16 kuelekea katika mechi hii, miongoni mwa wachezaji muhimu waliombukizwa ni Wahbi Khazri.