Pata taarifa kuu

Malalamiko ya Tunisia yatupwa, Cameroon imekuwa ya kwanza kufuzu hatua ya 16 bora

Malalamiko ya nchi ya timu ya taifa ya Tunisia, kuhusu tukio lililojitokeza wakati wa mchezo wake dhidi ya Mali na kupoteza mchezo huo kwa bao 1-0, yametupiliwa mbali na kamati ya maandalizi ya michuano ya mwaka huu.

Wachezaji wa Caqmeroon, Vincent Aboubakar na Eric Maxim Choupo Moting wakishangilia ushindi dhidi ya Ethiopia, ambapo Cameroon ilishinda kwa mabao 4-1.
Wachezaji wa Caqmeroon, Vincent Aboubakar na Eric Maxim Choupo Moting wakishangilia ushindi dhidi ya Ethiopia, ambapo Cameroon ilishinda kwa mabao 4-1. REUTERS - MOHAMED ABD EL GHANY
Matangazo ya kibiashara

Mali walikuwa wakongoza kwa bao 1-0 wakati mwamuzi kutoka Zambia, Janny Sikazwe, alipopuliza filimbi ya mwisho kuashiria kumalizika kwa mchezo dakika ya 85 kabla ya kufanya hivyo tena dakika ya 89 na sekunde 47, dakika tatu kabla ya kukamilika kwa muda wa nyongeza.

Tunisia ambao wakati huo walikuwa wakifanya jitihada za kurejesha goli hilo, walijikuta wakicheza pungufu kwa watu 10 uwanjani baada ya kufanya vurugu na mchezaji wao kuzawadiwa kadi nyekundu.

Mwamuzi wa Zambia, Janny Sikazwe, akibishana na kocha wa Tunisia, Mondher Kebaier, baada ya kumaliza mchezo wao kabla ya wakati. ilikuwa Januari 12, 2022.
Mwamuzi wa Zambia, Janny Sikazwe, akibishana na kocha wa Tunisia, Mondher Kebaier, baada ya kumaliza mchezo wao kabla ya wakati. ilikuwa Januari 12, 2022. REUTERS - MOHAMED ABD EL GHANY

Hata hivyo baada ya timu kutaarifiwa kuhusu kurejea uwanjani ili kumalizia dakika zilizobaki, timu ya Tunisia iligoma kurejesha timu uwanjani wakati Mali wao walikubali.

 

Baada ya kupitia malalamiko ya pingamizi ya Tunisia na pia ripoti za maofisa wote wa      mchezo, kamati ya maandalizi iliamua kutupilia mbali pingamizi lililowasilishwa na timu ya Tunisia na kuagiza matokeo kubakia 1-0 kwa timu ya Mali. Ilisema taarufa ya shirikisho la mpira Afrika, CAF.

Katika hatua nyingine timu ya taifa ya Cameroon, ilikuwa timu ya kwanza kufuzu kwenda hatua ya mtoano ya 16 bora, baada ya wachezaji wake Vincent Aboubakar na Karl Toko-Ekambi, kila mmoja kufunga mabao 2 katika ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Ethiopia.

Cameroon pia ilikuwa timu ya kwanza kufanikiwa kufunga goli zaidi ya 1 katika mchezo wa ufunguzi, ambapo walipata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Burkina Faso.

Kwa sasa wana alama tatu zaidi mbele ya Burkina Faso na Cape Verde, ambao walikutana siku ya Alhamisi na Burkina Faso kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Nchi ya Ethiopia ambao ni mabingwa wa taji hili mwaka 1962, hawakufanikiwa kupata sare wa ushindi ambao ungeweza kufufua matumaini yao ya kusonga mbele kwenye hatua ya mtoano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.