Pata taarifa kuu
UFARANSA-HAKI-SOKA

Soka: Benzema ahukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela katika kesi ya ngono

Mahakama ya Jinai ya Versailles imempata karim mostafa benzema, mchezaji wa Real Madrid na hatia ya kushiriki katika kosa la kujaribu kulaghai kupitia kanda ya ngono. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea Real Madrid amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na faini ya Euro 75,000.

Karim Benzema.
Karim Benzema. FRANCK FIFE AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Miaka sita baada ya kuanza kwa kesi ya ngono ya Mathieu Valbuena na karibu mwezi mmoja baada ya kesi yake ya jinai, Karim Benzema amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na faini ya Euro 75,000.

Mshambuliaji huyo wa Real Madrid, ambaye hakuhudhuria kesi hiyo ya siku tatu mwezi uliopita kutokana na ajenda ya michezo ya klabu yake, kwa mujibu wa mawakili wake, pia hakuwepo wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo. Leo usiku, Real inacheza mechi ya Ligi ya Mabingwa kwenye uwanja wa Sheriff Tiraspol huko Moldova.

Kwa madai ya kuhusika katika kisa cha kanda ya ngono, udukuzi wa video dhidi ya mchezaji kandanda Mathieu Valbuena mwaka 2015, upande wa mashtaka uliomba dhidi yake kifungo cha miezi 10 jela na faini ya euro 75,000. Wakati wa mashtaka, waendesha mashtaka walikumbusha jukumu la nyota huyo wa Ufaransa kama mfano, wa mtu ambaye ni "mbeba bendera, tumaini, mwenye sifa nzurina maadili mema".

"Karim Benzema alijihusisha na msisitizo katika kujaribu kumshawishi Mathieu Valbuena kukutana na mtu wake anayemuamini", imeleza mahakama.

Mawakili wa mshambuliaji huyo wa The Blues walitangaza mara moja kwamba mteja wao atakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo. Washtakiwa wengine wanne katika kesi hii iliyotikisa ulimwengu wa soka ya Ufaransa, Mahakama ya Jinai ya Versailles imetangaza hukumu za kuanzia miezi kumi na minane ya kifungo hadi miaka miwili na nusu jela. Karim Benzema alikuwa anakabiliwa na adhabu ya juu zaidi ya miaka mitano jela na faini ya euro 75,000.

Hukumu hiyo haipaswi kutilia shaka kurejea kwa Benzema katika timu ya Ufaransa, ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa miaka kadhaa kabla ya kurejea katika michuano ya Euro msimu wa joto wa 2021. Kwa vyovyote vile, "Benzema hatokataliwa kucheza katika klabu yake licha ya hukumu ya mahakama”, alionya rais wa Shirikisho la Soka la Ufaransa Noël Le Graët Novemba 10 katika gazeti la kila siku la Le Parisien.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.