Pata taarifa kuu
UFARANSA-SENEGAL-MICHEZO-LAMINE-RIADHAA-HAKI

Lamine Diack na mwanae kusikilizwa katika mahakama ya Paris

Mahakama jijini Paris nchini Ufaransa, leo Jumatatu itasikiliza kesi inayomkabili rais wa zamani wa Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF), Lamine Diack, raia wa Senegal  na mtoto wake Papa Massata Diack wanaotuhumiwa kwa mashtaka ya rushwa na utakatishaji wa fedha wakati akiwa uongozini kati ya mwaka 1999-2015.

Lamine Diack, mkuu wa zamani wa Shirikisho la Riadha la Kimataifa IAAF, ambaye anashutumiwa kupokea mamilioni ya fedha ili kuficha majibu ya vipimo vya dawa za kusisimua misuli ya Russia na kutakatisha pesa.
Lamine Diack, mkuu wa zamani wa Shirikisho la Riadha la Kimataifa IAAF, ambaye anashutumiwa kupokea mamilioni ya fedha ili kuficha majibu ya vipimo vya dawa za kusisimua misuli ya Russia na kutakatisha pesa. REUTERS/Jason Lee
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi uliofanywa na Ofisi ya mwendesha mashataka wa fedha nchini Ufaransa mwaka 2018 ni pamoja na madai kwamba Lamine Diack amechukua pesa kutoka Urusi kwa ajili ya kampeni za kisiasa za Senegal, na badala yake IAAF kusaidia kuficha makosa ya Urusi ya kutumia dawa za kusisimua misuli.

Mshauri wake wa masuala ya kisheria, wakili Habib Cissé, mwenye umri wa miaka 49, alichunguzwa pia, kwa tuhuma za kashfa ya rushwa pekee, pamoja na daktari Mfaransa Gabriel Dollé, ambaye alikuwa msimamizi wa kitengo kinacho pambana dhidi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini katika Shirikisho la kimataifa la Riadha hadi mwisho wa 2014.

Miaka michache iliyopita, Vladimir Putin alijihusisha sana katika michezo na hasa kwenye maandalizi ya mashindano kama Kombe la Dunia la Mpira wa Miguu la mwaka 2018, Michezo ya Olimpiki ya msimu wa baridi au Mashindano ya Dunia ya mwaka 2013 katika Riadha.

Lakini rais wa Urusi hakutaka tu kujihusisha na matukio hayo, bali pia alitaka kuona wanariadha wake wanafanya vizuri kwenye uwanja wa mashindan, amebaini Lukas Aubin, mtafiti wa jiografia na siasa, mtaalam wa masuala ya Urusi na michezo.

"Ili kuelewa muktadha wa kesi ya Lamine Diack, lazima uangaliye yaliyotkea mwaka 2000 katika ulimwengu wa michezo. Wakati Vladimir Putin alichukuwa hatamu ya uongozi wa nchi, alianza na mchakato mkubwa wa kuwashawishi viongozi mbalimbali katika michezo ya kimataifa ili kuweza kupata matukio makubwa zaidi ya michezo duniani: Michezo ya Sochi ya mwaka 2014, Kombe la Dunia la mwaka 2018 ... Mkakati huu ulifanya kazi! Lengo pia ilikuwa kunyakuwa ushindi katika michuano yote hiyo. Hapo sasa, ndipo kulianzishwa mchakato mkubwa wa kuanza kutumia madawa ya kusisimua misuli. Kwa hivyo hapo ndipo siasa iliingizwa katika michezo ya kimataifa kupitia mpatanishi wa Vladimir Putin, " amesema Lukas Aubin, mtafiti wa jiografia na siasa, mtaalam wa masuala ya Urusi na michezo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.