Pata taarifa kuu
KENYA-RIADHA-DUNIA-MASHINDANO

Kenya yamaliza ya pili baada ya Marekani katika mashindano ya riadha ya dunia

Mashindano ya riadha ya dunia ambayo yamekuwa yakiendelea jijini Doha nchini Qatar yamemalizika.

Mkenya Timothy Cheruiyot akishinda mbio za Mita 1500 kwa upande wa wanaume katika mashindano ya raidha ya dunia yaliyomalizika jijini Doha nchini Qatar
Mkenya Timothy Cheruiyot akishinda mbio za Mita 1500 kwa upande wa wanaume katika mashindano ya raidha ya dunia yaliyomalizika jijini Doha nchini Qatar www.iaaf.org
Matangazo ya kibiashara

Kama ilivyokuwa mwaka 2017 wakati wa mashindani kama haya, wakati yalipofanyika jijini London nchini Uingereza, Marekani imemaliza ya kwanza, huku Kenya ikiwa ya pili.

Marekani iliongoza  kwa  kupata medali 29, zikiwemo 14 za dhahabu, 11 za fedha na 4 za shaba.

Kenya ilimalizima mashindano hayo kwa kupata medali 11, zikiwemo tano za dhahabu  mbili za fedha na nne za shaba.

Miongoni mwa wanariadha wa Kenya waliopata medali ya dhahabu ni pamoja na Hellen Obiri mbio za Mita 5,000 kwa upande wa wanawake na Conseslus Kipruto Mita 3,000 kuruka viunzi na maji.

Jamaica ilimaliza ya tatu, kwa medali 12 huku Ethiopia ikimaliza katika nafasi ya 5 na Uganda ya tisa.

Mashindano yajayo ya dunia yatafanyika mjini Eugene, Oregon nchini Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.