Pata taarifa kuu
ULAYA-CORONA-AFYA-SOKA

Coronavirus: Ligi za Ulaya kurejelewa

Ligu  kuu za Ulaya  zikitarajiwa kurejelewa baada ya mlipuko wa virusi vya Corona, bado kuna hofu ya maabukizi ya virusi vya Corona miongoni mwa wachezaji, hatua inayoibua wasiwasi iwapo mechi zitachezwa.

Shirikisho la Soka nchini Ujerumani (DFB) limesema msimu huu utaanza, huku kukiwa na masharti ya kiafya ambayo yanapaswa kuzingatiwa kwa kutoruhusu mashabiki kuhudhuria uwanjani kuona mechi na wachezaji kupima virusi vya Corona.
Shirikisho la Soka nchini Ujerumani (DFB) limesema msimu huu utaanza, huku kukiwa na masharti ya kiafya ambayo yanapaswa kuzingatiwa kwa kutoruhusu mashabiki kuhudhuria uwanjani kuona mechi na wachezaji kupima virusi vya Corona. © REUTERS/Kai Pfaffenbach
Matangazo ya kibiashara

Ujurumani bado ina matumaini ya kuwa kileleni mwa ligi tano kuu za ulaya, huku Ufaransa ikitarajiwa kurejelea ligi yake kuanzia tarehe 16 mwezi huu bila mashabiki.

Hata hivyo ligi kuu ya Ujerumani maarufu Bundesliga, itarejelea mechi zake bila kuwa na mashabiki uwanjani tarehe 16 Mei.

Shirikisho la Soka nchini Ujerumani (DFB) limesema msimu huu utaanza, huku kukiwa na masharti ya kiafya ambayo yanapaswa kuzingatiwa kwa kutoruhusu mashabiki kuhudhuria uwanjani kuona mechi na wachezaji kupima virusi vya Corona.

Watu wapatao 300 wakiwemo wachezaji, wafanyakazi na maofisa ndio watakuwa ndani au karibu na uwanja wa mpira, siku mechi itakapochezwa.

Hiyo itakuwa mechi ya kwanza kuchezwa katika ligi la Ulaya kufuatia mechi nyingi kusitishwa kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona.

Ligi hii ilikuwa imesimasishwa tangu Machi 13. Vilabu vingi vilirejea kufanya mazoezi katikati ya mwezi Aprili, wachezaji wakiwa wanafanya mazoezi kwa makundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.