Pata taarifa kuu
DUNIA-CORONA-AFYA

Zaidi ya watu milioni 3.5 waambukizwa virusi vya Corona duniani

Maambukizi ya virusi vya Corona duniani yamepindukia milioni 3.5 leo Jumatatu, wakati idadi ya vifo vinavyosababishwa na janga hilo imeongezeka hadi zaidi ya 245,000, ingawa viwango vya maambukizi mapya na vifo vimepungua ikilinganishwa na mwezi uliopita, kulingana na ripoti ya shirika la habari la Reuters.

Ugonjwa wa Covid-19 umeathiri nchi mbalimbali dunia, huku uchumi ukidorora.
Ugonjwa wa Covid-19 umeathiri nchi mbalimbali dunia, huku uchumi ukidorora. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Visa vingi vilivyothibitishwa katika siku za hivi karibuni viliripotiwa katika ukanda wa Amerika ya Kaskazini na nchi za Ulaya, ingawa idadi ya kila siku ya maambukizi mapya inaongezeka katika ukanda wa Amerika ya Kusini, Afrika na Urusi.

Duniani kote, visa vipya 84,004 vilivyogunduliwa ndani ya masaa 24 yaliyopita, shirika la habari la Reuters limebaini, huku likijikita katika takwimu rasmi zilizotolewa na kila, idadi ambayo inafanya jumla ya visa duniani kote kufikia zaidi ya milioni 3.5.

Vifo vinavyotokana na mlipuko wa Covid-19, ugonjwa unaosababisha matatizo ya kupumua vimefikia jumla ya 245,992.

Kifo cha kwanza kiliripotiwa mnamo Januari 10 katikati mwa Uchina, huko Wuhan, jiji ambalo virusi vya Corona vilianzia mwezi Desemba mwaka jana.

Kiwango cha kila siku cha maambukizi ya virusi ulimwenguni kilisalia kati ya 2% na 3% wiki iliyopita, dhidi ya 13% katikati ya mwezi Machi, na kusababisha nchi nyingi kuanza kulegeza masharti ya watu kutotembea ili kuendeleza shughuli mbalimbali, wakati mgogoro wa kiafya umezorotesha uchumi wa dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.