Pata taarifa kuu
SOKA

Vlabu vya soka kutoka Kenya na Tanzania kuwania taji la Sportpesa

Vlabu vya soka kutoka nchini Tanzania na Kenya vinakutana jijini Dar es salaam kumenyana katika makala maalum ya kuwania taji la SportPesa Super Cup.

Picha ya ratiba ya michuano ya Sportpesa
Picha ya ratiba ya michuano ya Sportpesa pbs.twimg
Matangazo ya kibiashara

Vlabu vinavyoshriki katika michuano hii ni pamoja na AFC Leopards, Tusker FC, Gor Mahia na Nakuru All Stars kutoka nchini Kenya.

Wawakilishi wa Tanzania ni pamoja na Singida United, Yanga FC, Jang’ombe Boys FC na Simba SC.

Kampuni ya Sportpesa inayofadhili ligi kuu ya Kenya lakini baadhi ya vlabu nchini Tanzania, imekuja na michuano hii kwa lengo la kujitangaza zaidi katika ukanda wa Afrika Masharki na Kati.

Ratiba Juni 5 2017

  • AFC Leopards (Kenya) vs Singida United (Tanzania)
  • Yanga (Tanzania) vs Tusker FC (Kenya)

Jumanne Juni 6 2017

  • Gor Mahia (Kenya) vs Jang’ombe Boys FC (Zanzibar)
  • Simba SC (Tanzania) vs Nakuru All Stars (Kenya)

Tuzo

  • Mshindi -Dola za Marekani 30,000​
  • Mshindi wa pili- Dola za Marekani 10,000
  • Nusu fainali- Dola za Marekani 5,000
  • Robo fainali-Dola za Marekani 2,500
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.