Pata taarifa kuu
michezo

Simba yaibuka bingwa dhidi ya Prison

Masaa 24 yalitosha kwa klabu kubwa nchini Tanzania Simba kujiweka mstarini kwa kujipatia magoli 2 dhidi ya 1 la Prison kutoka Mbeya Tanzania katika mechi iliyotoa burudani katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Kikosi cha Simba ambacho kimeibuka na ushindi dhidi ya Prison ya Mbeya Tanzania
Kikosi cha Simba ambacho kimeibuka na ushindi dhidi ya Prison ya Mbeya Tanzania liwazozito.blogspot.com
Matangazo ya kibiashara

Simba ilijituma vema tangu kuanza kwa michuano ya kandanda ambapo ilionesha ubabe wake katika mechi nne mfululizo.

Mechi hiyo iliyotawaliwa na ushindani mkubwa ktoka kwa timu zote mbili ambazo zilianza kwa kufanya mashambulizi ya kushtukiwa ambapo Prisons ilitangulia kupata bao dakika ya sita likifungwa na Lugano mwangama baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Simba.

Hata hivyo bao la Prison halikuivunja nia ya Simba kufanya vizuri baada ya kipindi cha kwanza Felix Sunzu kudaka mpira na kuutandika katika wavu wa Prisons huku mlinda mlango wa timu hiyo David Abdalah akishindwa kuhimili na kuruhusu bao lililoiandikia Simba bao.
 

Mechi ingine inatarajiwa kufanyika jumatano ijayo ambapo klabu hiyo itavaana na Yanga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.