Pata taarifa kuu
NEWCSTLE-SOKA-MICHEZO

Cheick Tiote, mchezaji wa Cote d'Ivoire afariki dunia

Cheick Tiote, mchezaji wa kimataifa wa Cote d'Ivoire ambae ni kiungo wa zamani wa klabu ya Newcastle United amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 30 baada ya kuzimia wakati wa mazoezi nchini China, msemaji wa Tiote amesema.

Kiungo wa kiimataifakutoka Cote d'Ivoiret Cheick Tiote, hapa ilikua Oktoba 13, 2014 katika mji wa Abidjan, wakati wa mechi ya kufuzu kwa CAN 2015 dhidi DRC.
Kiungo wa kiimataifakutoka Cote d'Ivoiret Cheick Tiote, hapa ilikua Oktoba 13, 2014 katika mji wa Abidjan, wakati wa mechi ya kufuzu kwa CAN 2015 dhidi DRC. ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Cheick Tiote aliichezee Newcastle mechi 138 kwa miaka saba, na alihamia klabu ya Beijing Enterprises mwezi Februari mwaa huu.

Cheick Tiote alizaliwa nchini Cote d'Ivoire na alikuwa kwenye kikosi kilichoshinda Kombe la Mataifa ya Afrika 2015.

Alianza kucheza soka ya kulipwa nchini Ubelgiji katika klabu ya Anderlecht mwaka 2005 kabla ya kuhamia FC Twente ya Uholanzi ambapo alicheza mechi 86 na kushinda taji la ligi ya Eredivisie msimu wa 2009-10 chini ya meneja Steve McLaren.

Tiote alihamia Newcastle mwaka 2010 baada ya kununuloiwa Euro milioni 3.5.

msemaji wake alisema "ni kwa huzuni kubwa ambapo ninathibitisha kwamba Cheick Tiote alifariki mapema leo baada ya kuzimia wakati wa mazoezi,".

Na kuongeza "hatuwezi kusema zaidi kwa sasa na tunaomba kwamba familia yake iheshimiwe kipindi hiki kigumu. Tunaomba maombi yenu."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.