Pata taarifa kuu
AFRIKA-CAF-SOKA-AFCON 2015-MICHEZO

AFCON 2015: timu 16 zawekwa katika makundi

Timu kumi na sita zitakazoshiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika nchini Equatorial Guinea zimepangwa katika makundi manne Jumatano Novemba 3, wakati ambapo zinasalia siku chache ili michuano hiyo ianze.

Michel Dussuyer (kushoto), meneja wa Gunea, pamoja na Henryk Kasperczak, kocha wa Mali wakizungumza. timu hizo zitakutana katika michuano ya AFCON 2015.
Michel Dussuyer (kushoto), meneja wa Gunea, pamoja na Henryk Kasperczak, kocha wa Mali wakizungumza. timu hizo zitakutana katika michuano ya AFCON 2015. RFI/ David Kalfa
Matangazo ya kibiashara

Wenyeji Eqauatorial Guinea na Congo zitacheza mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo. Kundi D ambalo linaundwa na Cote d'Ivoire , Mali, Cameroon na Uinea linaonekana kuwa ngumu zaidi ikilinganishwa na makundi mengine.

Kundi A inaundwa na Equatorial Guinea, Burkina Faso, Gabon, Congo
Kundi B inaundwa na Zambia, Tunisia, Cape Verde, DR Congo
Kundi C inaundwa na Ghana, Algeria, South Africa, Senegal
Kundi D inaundwa na Ivory Coast, Mali, Cameroon, Guinea

Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika imepangwa kuanza Januari 17 hadi Februari 8 mwaka 2015.

Nigeria, ambayo ni mabingwa watetezi, Angola pamoja na pamoja na Misri zilijikuta ziliondolewa katika michuano hiyo baada ya kushindwa kufanya vizuri katika michuano iliyokua ikichezwa hiviu karibuni.

Equatorial Guinea ilichukua nafasi ya Morocco, baada ya Morocco kujiengua kwenye nafasi hiyo ya kuandaa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015, ikihofia mambukizi ya virusi vya Ebola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.