Droo ya michuano ya AFCON 2019 yatangazwa
Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limetangaza droo ya michuano ya kufuzu kucheza kombe la mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Wenyeji wa michuano hii Cameroon, wamepangwa katika kundi moja la B na mabingwa mwaka 1976 Morocco, Malawi na Comoros au Mauritius.
Mabingwa mara saba Misri, watakutana na wapinzani wao wa Afrika Kaskazini Tunisia walioshinda taji hili mwaka 2004.
Nigeria itamenyana na mabingwa mwaka 1996 Afrika Kusini.
Kundi la G, nchi jirani Congo itamenyana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Michuano hii itaanza kuchezwa kati ya mwezi Machi na Novemba mwaka 2018, nyumbani na ugenini.
Droo kamili:
A: Senegal, Equatorial Guinea, Sudan, Sao Tome /Madagascar
B: Cameroon, Morocco, Malawi, Comoros/Mauritius
C: Mali, Gabon, Burundi, Djibouti/South Sudan
D: Algeria, Togo, Benin, The Gambia
E: Nigeria, South Africa, Libya, Seychelles
F: Ghana, Ethiopia, Sierra Leone, Kenya
G: DR Congo, Congo, Zimbabwe, Liberia
H: Ivory Coast, Guinea, Central African Republic, Rwanda
I: Burkina Faso, Angola, Botswana, Mauritania
J: Tunisia, Egypt, Niger, Swaziland
K: Zambia, Mozambique, Guinea-Bissau, Namibia
L: Cape Verde, Uganda, Tanzania, Lesotho