Pata taarifa kuu
AFCON 2017

Uchambuzi wa mataifa yanayoshiriki AFCON 2017 nchini Gabon

Fainali ya 31 kuwania taji la mataifa bingwa barani  Afrika, inaanza siku ya Jumamosi, Januari tarehe 14 nchini Gabon. Mataifa 16, yanashiriki katika michuano hii itakayochezwa katika miji minne ya Libreville, Franceville, Oyem na Port Gentil. Mataifa yatakayoshiriki  yamepangwa katika makundi manne. Tunakuletea uchambuzi wa kina wa timu zote.  

Makundi ya timu zitakazocheza michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwakani nchini Gabon.
Makundi ya timu zitakazocheza michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwakani nchini Gabon. cafonline.com/Youtube
Matangazo ya kibiashara

KUNDI A.

Kikosi cha Gabon.
Kikosi cha Gabon.

Kundi A lina jumla ya timu nne, wamo wenyeji wa michuano ya mwaka huu, timu ya taifa ya Gabon, Guinea-Bissau, Cameroon na Burkina Faso.Timu ya taifa ya Gabon:

Timu ya taifa ya Gabon inashiriki michuano ya mwaka huu kama nchi mwenyeji. Timu hii imeshawahi kushiriki mara 6 kwenye michuano hii, na mwaka huu itakuwa ni mara yake ya .

Kwa mara ya kwanza Gabon ilishiriki michuano hii mwaka 1994 na kuishia kwenye hatua ya makundi.

Lakini mwaka 1996 baada ya kufanya vibaya mwaka 94, Gabon ilifika katika hatua ya robo fainali, mafanikio ambayo yalijirudia katika michuano ya mwaka 2012 ambapo ilikuwa nchi mwenyeji na Equatorial Guinea na kufika katika hatua ya robo fainali.

Jina la Utani la timu hii ni “Panthers”, kocha mkuu wa timu hii ni Jose Antonio Camacho.

Kikosi kamili cha Gabon: Kwenye mabano ni timu wanazochezea.

Makipa:
Anthony Mfa Mezui (clubless), Yves Stephane Bitseki Moto (Mounana), Didier Ovono (Ostend/BEL)

Mabeki:
Aaron Appindangoye (Laval/FRA), Bruno Ecuele Manga (Cardiff City/WAL), Franck Perrin Obambou (Stade Mandji), Johann Serge Obiang (Troyes/FRA), Benjamin Ze Ondo (Mosta/MAL), Lloyd Palun (Red Star/FRA), Andre Biyogho Poko (Karabukspor/TUR), Yoann Wachter (Sedan/FRA)

Viungo:
Guelor Kanga Kaku (Red Star/SRB), Mario Lemina (Juventus/ITA), Levy Clement Madinda (Nastic Tarragona/ESP), Didier Ndong (Sunderland/ENG), Junior Serge Martinsson Ngouali (Brommapojkarna/SWE), Merlin Tandjigora (Meixian Hakka/CHN), Samson Mbingui (Raja Casablanca/MAR)

Washambuliaji:
Serge Kevyn Aboue Angoue (Uniao Leiria/POR), Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund/GER, capt), Cedric Ondo Biyoghe (Mounana), Denis Athanase Bouanga (Tours/FRA), Malick Evouna (Tianjin Teda/CHN).

Nahodha wa kikosi hiki ni, Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund/GER).

Timu ya Taifa ya Guinea-Bissau:

Kikosi cha Guinea-Bissau
Kikosi cha Guinea-Bissau


Hii ni mara ya kwanza kwa timu ya taifa ya Guinea-Bissau, kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika. Wakati wa mechi za kufuzu, Guinea-Bissau ilimaliza ya kwanza kwenye kundi lake kwa kuwa na alama 10.

Kama ilivyofanya katika hatua ya makundi kufuzu kucheza fainali za mwaka huu, ndivyo ambavyo wadadisi wa soka wanaona kuwa huenda timu hii ikatengeneza historia kwenye michuano ya mwaka huu na pengine kuvuka hatua ya makundi.

Kikosi cha Guinea-Bissau, kinaongozwa na kocha, Bassirou CANDE.

Jina la utani la timu hii ni “Djurtus”

Kikosi Kamili cha timu ya taifa ya Guinea-Bissau: Kwenye mabano ni timu wanazochezea.

Makipa: Papa Mbaye (Orellana/ESP), Jonas Mendes (Salgueiros/POR), Edouard Mendy (Reims/FRA)

Mabeki: Mama Balde (Sporting Lisbon B/POR), Mamadu Cande (Tondela/POR), Eliseu Cassama (Rio Ave/POR), Eridson (Freamunde/POR), Emmanuel Mendy (Ceahlaul Piatra Neamt/ROU), Formose Mendy (Red Star/FRA), Rudinilson Silva (Lechia Gdansk/POL), Agostinho Soares (Sporting Covilha/POR), Juary Soares (Mafra/POR)

Viungo: Toni Silva, Zezinho (both Levadiakos/GRE), Abudu (Operario/POR), Aldair (Olhanense/POR), Bocundji Ca (Paris FC/FRA, capt), Abel Camara (Belenenses/POR), Idrissa Camara (Avellino/ITA), Francisco Junior (Stromsgodset/NOR), Frederic Mendy (Ulsan Hyundai/KOR), Jean-Paul Mendy (Quevilly-Rouen/FRA), Pele (Benfica B/POR), Piqueti (Sporting Braga B/POR), Leocísio Sami (Akhisar Belediyespor/TUR), Naní Soares (Gil Vicente/POR), Yazalde (Rio Ave/POR), Ze Turbo (Tondela/POR).

Washambuliaji:Guti Almada (Real Queluz/POR), Edelino Ie (Sporting Braga B/POR), Joao Mario (Chaves/POR), Mesca (AEL Limassol/CYP), Bruno Preira (Colomiers/FRA), Sana (Academico Viseu/POR)
Nahodha wa timu hii ni, Bocundji Ca (Paris FC/FRA)

 
Timu ya taifa ya Cameroon:

Timu ya taifa ya Cameroon
Timu ya taifa ya Cameroon

Timu ya taifa ya Cameroon, imeshawahi kushiriki michuano hii mara 17, na michuano ya mwaka huu itakuwa ni mara yake ya 18 kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika.

Kwa mara ya kwanza timu hii ilishiriki kombe hili mwaka 1970 na kuishia hatua ya makundi.

Cameroon imewahi kutwaa taji la Afrika mara nne (4), mwaka 1984, 1988, 2000 na 2002. Iliwahi kushika nafasi ya pili mara mbili, mwaka 1986 na mwaka 2008. Imewahi pia kufika katika hatua ya nusu fainali mara moja nayo ilikuwa ni mwaka 1992.

Cameroon ilimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye kundi M ikiwa na alama 14. Jina la utani la timu hii ni “Indomitable Lions” ikiwa na maana ya Simba wasiofugika.

Kocha mkuu wa timu hii ni Mbelgiji, BROOS Hugo.

Kikosi kamili cha Cameroon: Kwenye mabano ni timu wanazochezea.

Makipa: Guy-Roland Ndy Assembe (Nancy/FRA), Jules Goda (Ajaccio/FRA), Georges Mbokwe (Coton Sport), Andre Onana (Ajax Amsterdam/NED), Fabrice Ondoa (Sevilla/ESP)

Mabeki:
Henri Bedimo (Marseille/FRA), Aurelien Chedjou (Galatasaray/TUR), Fai Collins (Standard Liege/BEL), Mohamed Djeitei (Nastic Tarragone/ESP), Ernest Mabouka (Zilina/SVK), Joel Matip (Liverpool/ENG), Michael Ngadeu Ngadjui (Slavia Prague/CZE), Jonathan Ngwem (Progresso Sambizanga/ANG), Nicolas Nkoulou (Lyon/FRA), Allan Nyom (West Bromwich Albion/ENG), Ambroise Oyongo (Impact Montreal/CAN), Maxime Poundje (Bordeaux/FRA), Adolphe Teikeu (Sochaux/FRA)

Viungo:
Ibrahim Amadou (Lille/FRA), Franck Zambo Anguissa (Marseille/FRA), Franck Boya (Apejes Academy), Arnaud Djoum (Hearts/SCO), Franck Kom (Karlsruhe/GER), Georges Mandjeck (Metz/FRA), Sebastien Siani (Ostend/BEL)

Washambuliaji:
Anatole Abang (New York Red Bulls/USA), Vincent Aboubakar (Besiktas/TUR), Christian Bassogog (Aalborg/DEN), Eric-Maxim Choupo-Moting (Schalke/GER), Benjamin Moukandjo (Lorient/FRA), Clinton Njie (Marseille/FRA), Edgar Salli (Saint-Gall/SUI), Robert Ndip Tambe (Spartak Trnava/SVK), Karl Toko-Ekambi (Angers/FRA), Jacques Zoua (Kaiserslautern/GER)


Timu ya Taifa ya Burkina Faso:

Kikosi cha Burkina Faso
Kikosi cha Burkina Faso


Hii ni mara ya kumi (10) kwa timu ya taifa ya Burkina Faso kushiriki fainali za kombe la mataifa ya Afrika, mara ya kwanza kwa Burkina Faso kushiriki michuano hii ilikuwa ni mwaka 1970.

Mwaka 1998 Burkina Faso kwa mara ya kwanza ilimaliza kwenye nafasi za juu wakati walipoandaa fainali hizi na kumaliza katika nafasi ya nne. Lakini nafasi ya kipekee na mafanikio makubwa iliyowahi kupata timu hii ni mwaka 2013 ambapo ilifika kwenye hatua ya fainali.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Burkina Faso ni Paulo Duarte, raia wa Ureno. Jina la utani la timu hii ni “Les Étalons” Ikiwa na maana ya Farasi.

Kikosi kamili cha Burkina Faso: Kwenye mabano ni timu wanazochezea.

Makipa: Herve Koffi (ASEC/CIV), Moussa Germain Sanou (Beauvais/FRA), Aboubacar Sawadogo (Kadiogo)

Mabeki: Ernest Congo (Khemisset/MAR), Yacouba Coulibaly (Bobo), Issoufou Dayo (Berkane/MAR), Bakary Kone (Malaga/ESP), Souleymane Kouanda (ASEC/CIV), Issoumaila Lengani (Happoel Ashkelon/ISR), Patrick Malo (Smouha/EGY), Issouf Paro (Santos/RSA), Steeve Yago (Toulouse/FRA)

Viungo: Cyrille Bayala (Sheriff Tiraspol/MDA), Adama Guira (Lens/FRA), Charles Kabore (Krasnodar/RUS, capt), Prejuce Nacoulma (Kayserispor/TUR), Bakary Sare (Moreirense/POR), Blati Toure (Omonia Nicosia/CYP), Abdoul Razack Traore (Karabuspor/TUR), Alain Traore (Kayserispor/TUR), Bertrand Traore (Ajax Amsterdam/NED), Jonathan Zongo (Almeiria/ESP)

Washambuliaji: Aristide Bance (ASEC/CIV), Banou Diawara (Smouha/EGY), Jonathan Pitroipa (Al Nasr/UAE)

KUNDI B:

Kundi B nalo lina jumla ya timu nne, ambapo kuna timu ya taifa ya Senegal, Algeria, Tunisia na Zimbabwe.

Timu ya Taifa ya Senegal:

Kikosi cha Senegal
Kikosi cha Senegal


Timu ya taifa ya Senegal, imeshiriki michuano hii mara kumi na tatu (13) na katika michuano ya mwaka huu itakuwa ni mara yake ya kumi na nne (14). Mwaka 2002 timu hii ilifanikiwa kucheza hatua ya fainali lakini haikufanikiwa kutwaa taji hili. Mwaka 1990 na mwaka 2006 timu ya taifa ya Senegal ilifanikiwa kufika kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hii.

Senegal ilimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye kundi K. Kwa mara ya kwanza timu hii ilifuzu kucheza michuano ya Afrika mwaka 1965.

Kocha mkuu wa kikosi hiki ni mzawa, Cisse Aliou. Jina la utani la timu hii ni “Teranga Lions” ikiwa na maana ya Simba wa Teranga.

Kikosi kamili cha Senegal: Kwenye mabano ni timu wanazochezea.

Makipa:Abdoulaye Diallo (Caykur Rizespor/TUR), Khadim N'Diaye (Horoya/GUI), Pape Seydou N'Diaye (Niarry Tally)

Mabeki: Saliou Ciss (Valenciennes/FRA), Lamine Gassama (Alanyaspor/TUR), Kalidou Koulibaly (Napoli/ITA), Cheikh M'Bengue (Saint-Etienne/FRA), Kara Mbodj (Anderlecht/BEL), Zargo Toure (Lorient/FRA)

Viungo: Mohamed Diame (Newcastle/ENG), Papakouli Diop (Espanyol/ESP), Idrissa Gueye (Everton/ENG), Cheikhou Kouyate (West Ham/ENG, capt), Papa Alioune Ndiaye (Osmanlispor/TUR), Cheikh N'Doye (Angers/FRA), Henri Saivet (Saint-Etienne/FRA)

Washambuliaji: Keita Balde (Lazio/ITA), Famara Diedhiou (Angers/FRA), Mame Biram Diouf (Stoke/ENG), Moussa Konate (Sion/SUI), Sadio Mane (Liverpool/ENG), Ismaila Sarr (Metz/FRA), Moussa Sow (Fenerbahce/TUR)

Timu ya Taifa ya Algeria:

Kikosi cha Algeria
Kikosi cha Algeria

Timu ya taifa ya Algeria imeshiriki michuano hii mikubwa barani Afrika kwa mara 16 na michuano ya mwaka huu inakuwa ni mara yake ya 17, na mara ya kwanza kushiriki michuani hii ilikuwa ni mwaka 1968.

Mafanikio makubwa ambayo Algeria imeyapata toka ilipoanza kushiriki michuano hii, ni kufanikiwa kutwaa taji hili mwaka 1990, ikamaliza kwenye nafasi ya tatu katika michuano ya mwaka 1984 na 1988, ikafika hatua ya nusu fainali katika michuano ya mwaka 1982 na 2010.

Algeria ilimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye kundi J kwa alama 16. Jina la utani la timu hii ni “Les Fennecs”.

Kocha mkuu wa kikosi cha Algeria ni Mbelgiji, George Leekens.

Kikosi kamili cha Algeria: Kwenye mabano ni timu wanazochezea.

Makipa: Malik Asselah (JS Kabylie), Rais M'Bolhi (Antalyaspor/TUR), Chemseddine Rahmani (Mouloudia Bejaia)

Mabeki: Mohamed Benyahia, Mohamed Meftah (both USM Alger),Hichem Belkaroui (Esperance/TUN), Mokhtar Belkhiter (Club Africain/TUN), Ramy Bensebaini (Rennes/FRA), Liassine Cadamuro (Servette/SUI), Faouzi Ghoulam (Napoli/ITA), Aissa Mandi (Real Betis/ESP), Djamel Mesbah (Crotone/ITA)

Viungo: Mehdi Abeid (Dijon/FRA), Nabil Bentaleb (Schalke/GER), Yacine Brahimi (Porto/POR), Rachid Ghezzal (Lyon/FRA), Adlene Guedioura (Watford/ENG), Riyad Mahrez (Leicester City/ENG), Saphir Taider (Bologna/ITA)

Washambuliaji:Baghdad Bounedjah (Al Sadd/QAT), Sofiane Hanni (Anderlecht/BEL), Islam Slimani (Leicester/ENG), El Arabi Hillel Soudani (Dinamo Zagreb/CRO)

Timu ya Taifa ya Tunisia:

Kikosi cha Tunisia
Kikosi cha Tunisia


Timu ya taifa ya Tunisia imeshiriki michuano hii ya kombe la mataifa ya Afrika mara 16, na michuano ya mwaka huu itakuwa ni mara yake ya 17.

Mwaka 1965 Tunisia ilimaliza katika nafasi ya 2 baada ya kufika fainali, sawa na mwaka 1996, lakini mwaka 2004 Tunisia ilifanikiwa kutwaa taji hili la Afrika.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tunisia ni Mpoland, Henryk Kasperczak. Jina la utani la timu hii ni “Les Aigles de Carthage”.

Kikosi kamili cha timu ya Tunisia: Kwenye mabano ni timu wanazochezea.

Makipa: Moez Ben Cherifia (Esperance), Rami Jeridi (Sfaxien), Aymen Mathlouthi (Etoile Sahel, capt), Farouk Ben Mustapha (Club Africain)

Mabeki: Ghazi Abderrazak, Zied Boughattas, Hamdi Nagguez (all Etoile Sahel), Chamseddine Dhaouadi, Ali Machani, Iheb Mbarki (all Esperance), Oussama Haddadi, Bilel Ifa (both Club Africain), Aymen Abdennour (Valencia/ESP), Slimen Kchok (CA Bizertin), Ali Maaloul (Al-Ahly/EGY), Hamza Mathlouthi (Sfaxien), Mohamed Ali Yaakoubi (Caykur Rizespor/TUR), Syam Ben Youssef (Caen/FRA)

Viungo: Mohamed Amine Ben Amor, Hamza Lahmar, Iheb Msakni (all Etoile Sahel), Saad Bguir, Ferjani Sassi (both Esperance), Larry Azouni (Nimes/FRA), Anis Ben Hatira (Darmstadt/GER), Wahbi Khazri (Sunderland/ENG), Issam Ben Khemis (Lorient/FRA), Yassine Meriah (Sfaxien), Youssef Msakni (Lekhwiya/QAT), Abdelkader Oueslati (Club Africain), Naim Sliti (Lille/FRA)

Washambuliaji: Ahmed Akaichi (Ittihad Jeddah/KSA), Khaled Ayari (Paris FC/FRA), Nejmeddin Daghfous (Wurzburg/GER), Hamdi Harbaoui (Anderlecht/BEL), Issam Jebali (Elfsborg/SWE), Saber Khalifa (Club Africain), Ahmed Khalil (Al Ahly/UAE), Taha Yassine Khenissi (Esperance), Idriss Mhirsi (Red Star/FRA), Yoann Touzghar (Auxerre/FRA).

Nahodha wa kikosi hiki ni Yassine Chikhaoui.

 Timu ya Taifa ya Zimbabwe:

Kikosi cha Zimbabwe
Kikosi cha Zimbabwe


Timu ya taifa ya Zimbabwe imewahi kushiriki michuano hii mara mbili (2), na michuano ya mwaka huu itakuwa ni mara yake ya tatu (3) kushiriki.

Kwa mara ya kwanza Zimbabawe ilifuzu kwenye michuano hii mwaka 2004, na toka wakati huo haijawahi kupata mafanikio makubwa kwenye michuano hii, zaidi ya kuishia katika hatua ya makundi ya michuano hii mikubwa barani Afrika.

Zimbabwe ilimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye kundi L ikiwa na alama 11. Jina la utani la timu hii ni “Warriors” ikiwa na maana ya mashujaa.

Kocha mkuu wa timu hii ni mzawa, Pasuwa Calistus. Nahodha wa timu ya taifa ya Zimbabwe ni Willard Katsande.

Kikosi kamili cha timu ya taifa ya Zimbabawe: Kwenye mabani ni timu wanazochezea.

Makipa: Donovan Bernard (How Mine), Nelson Chadya (Ngezi Platinum), Takabva Mawaya (Hwange), Tatenda Mkuruva (Dynamos)

Mabeki: Teenage Hadebe, Lawrence Mhlanga (both Chicken Inn), Onismor Bhasera (SuperSport Utd/RSA), Liberty Chakoroma (Ngezi Platinum), Bruce Kangwa (Azam/TAN), Oscar Machapa (V Club/COD), Blessing Moyo (Maritzburg Utd/RSA), Elisha Muroiwa (Dynamos), Tendai Ndlovu (Highlanders), Costa Nhamoinesu (Sparta Prague/CZE), Hardlife Zvirekwi (CAPS Utd)

Viungo: Kudakwashe Mahachi, Danny Phiri (both Golden Arrows/RSA), Khama Billiat (Mamelodi Sundowns/RSA), Talent Chawapiwa (ZPC Kariba), Ronald Chitiyo (Harare City), Willard Katsande (Kaizer Chiefs/RSA, capt), Raphael Kutinyu (Chicken Inn), Marshall Mudehwe (FC Platinum), Marvelous Nakamba (Vitesse Arnhem/NED)

Washambuliaji: Tinotenda Kadewere (Djurgardens/SWE), Cuthbert Malajila (Wits/RSA), Nyasha Mushekwi (Dalian Yifang/CHN), Knowledge Musona (Ostend/BEL), Tendai Ndoro (Orlando Pirates/RSA), Evans Rusike (Maritzburg/RSA), Mathew Rusike (Helsingborgs/SWE).

Kikosi cha DRC
Kikosi cha DRC

Timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, maarufu kama Leopard, inarejea katika michuano ya kutafuta ubingwa wa Afrika kwa mara ya 16.

Mara ya kwanza kwa DRC kushiriki katika michuano hii mikubwa barani Afrika, wakati huo ikiwa inaitwa Zaire, ilikuwa ni mwaka 1965.

Mwaka 2015,ndio mara ya mwisho kwa nchi hii kushiriki katika michuano hii ilipofanyika nchini Equatorial Guinea na kumaliza katika nafasi ya tatu.

Safari ya kwenda Gabon
Mabingwa walioshinda taji hili mara mbili, mwaka 1968 na 1974, walimaliza wa kwanza katika kundi lao la B walilopangwa na Angola, Madagascar na Jamhuri ya Afrika ya Kati, kutafuta tiketi ya kwenda Gabon.

Nchini Gabon, Leopard ambayo ni ya 48 duniani, imepangwa katika kundi moja la C na mabingwa watetezi Ivory Coast, Morocco na Togo.

Leopard inatumai kuwa itamaliza katika mbili bora ili kufuzu katika hatua ya mwondoano na kutafuta ubingwa ambao mara ya mwisho walishinda miaka 42 iliyopita.

Kocha
DR Congo inafuzwa na Florent Ibenge mwenye umri wa miaka 55, na ni miongoni mwa makocha wanne pekee wa nyumbani wanaofunza mataifa yao.

Makocha wengine wa nyumbani wanaofunza nchi zao ni kutoka Zimbabwe, Guinea Bissau na Senegal.

Ibenge alianza kuifunza Leopard mwezi Agosti mwaka 2014, baada ya kuchukua nafasi ya raia mwenzake Jean Santos Muntubilla.

Atakumbukwa kuiongoza DRC kushinda taji la Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani CHAN mwaka 2016, michuano iliyofanyika nchini Rwanda.

Kikosi
Kikosi cha sasa cha Leopard kinawajumuisha wachezaji wengi walioshinda taji la CHAN kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani ,akiwemo kipa wa klabu ya TP Mazembe Ley Matampi, Issama Mpeko, Merveille Bokadi, Jonathan Bolingi, Elia Meschak na Joyce Lomalisa.

Hata hivyo, Ibenge itamkosa mchezaji wa Everton Yannick Bolasie, ambaye anauguza majeraha.

Kikosi kamili:

Makipa: Kiassumbua Joel (whollen fc/ suisse), Matampi Vumi Ley (TP Mazembe/ RD Congo), Kudimbana Nicaise (Antwerp/ Ubelgiji)

Mabeki: Issama Mpeko Djo (TP Mazembe/ RD Congo), Bope Bokadi Merveille (TP Mazembe/ RD Congo), Lomalisa Mutambala (AS V.Club/ RD Congo), Ikoko Jordan (Guingamp/ Ufaransa), Tisserand Marcel (Fc Ingolstadt/ Ujerumani), Zakuani Gabriel (Peterborough/ Uingereza), Fabrice N’sakala (Alanyaspor/ Uturuki)

Viungo wa Kati: Mulumba Remy (Gazele Fc Ajaccio/ Ufaransa), Mpoku Paul-Jose (Panathinaikos/ Ugiriki), Herve Kage  (Kv Courtrai/ Ubelgiji), Mbemba Chancel (Newcastle/ Uingereza), Youssuf Mulumbu (Norwich City/ Uingereza), Maghoma Jacques (Birmingham/ Uingereza), Kebano Neeskens (Fulham/ Uingereza)

Washambuliaji: Mubele Ndombe Firmin (Al Ahli Doha/ Qatar), Junior Kabananga (Astana / Kazakhstan), Jeremy Bokila Loteteka (Al Quarittyah/ Qatar), Bakambu Cedrick (Villareal/ Uhispania), Bolingi Mpangi Jonathan (Tp Mazembe/ DRC), Botaka Jordan (Charlton/ Uingereza), Mbokani Bezua Dieumerci (Hull City/ Uingereza)

Maandalizi
Leopard inapiga kambi nchini Cameroon ikisubiri mchuano wake wa ufunguzi dhidi ya Morocco katika uwanja wa d'Oyem tarehe 16 Januari.

 

IVORY COAST

Kikosi cha Ivory Coast
Kikosi cha Ivory Coast

Ivory Coast au Cote Dvoire, ndio mabingwa watetezi wa taji hili, waliloshinda mwaka 2015 nchini Equitorial Guinea baada ya kusubiri kwa muda mrefu tangu 1992.
Haya ni makala ya 22 ya michuano hii katika historia yake ya michuano hii ya mataifa bingwa.

Safari ya kwenda Gabon
The Elephants kama wanavyofahamika kwa jina la utani, walifuzu katika michuano hii, baada ya kushinda kundi la I kwa alama 6, nyuma ya Sierra Leone iliyomaliza kwa alama 5 huku Sudan ikiwa ya mwisho kwa alama 4.

Hili ni kundi ambalo lilitoa mshindi mmoja kwa sababu kulikuwa tu na mataifa matatu, yaliyoshiriki katika michuano hii ya kufuzu.

Kocha
Ivory Coast inafunzwa na Mfaransa Michel Dussuyer.

Kabla ya kupewa kibarua nchini Ivory Coast, alikuwa anaifunza timu ya taifa ya Guinea kati ya mwaka 2010-2013 na baadaye mwaka 2014-2015.

Kocha huyu mwenye umri wa miaka 57, amewahi pia kuifunza Benin kati ya mwaka 2008-2010.

Nchi yake ya kwanza kuifunza ilikuwa ni Guinea mwaka 2002.

Ni kocha ambaye ametumia kuifunza Guinea kwa muda wa miaka 7.

Kikosi
Ivory Coast inajivunia na wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa katika mataifa mengi ya bara Ulaya. Ni kikosi cha wachezaji wanaotajwa kuwa na vipaji vya hali ya juu.

Hata hivyo, Yao Gervinho  atakosa michuano ya mwaka huu kwa sababu ya jeraha la goti analouguza na anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa miezi sita.

Yaya Toure mchezaji wa Manchester City yeye amestaafu kucheza soka la Kimataifa.

Kikosi kamili:
Makipa: Sylvain Gbohouo (TP Mazembe/COD), Ali Badra Sangare (Tanda), Mande Sayouba (Stabaek/NOR)

Mabeki: Serge Aurier (PSG/Ufaransa), Mamadou Bagayoko (Saint-Trond/UBELGIJI), Eric Bailly (Manchester Utd/UINGEREZA), Simon Deli (Slavia Prague/CZECH), Ousmane Viera Diarrassouba (Adanaspor/UTURUKI), Wilfried Kanon (ADO Hague/Uholanzi), Lamine Kone (Sunderland/Uingereza), Adama Traore (Basel/Uswizi)

Viungo wa Kati: Victorien Angban (Granada/Uhispania), Geoffrey Serey Die (Basel/Uswizi), Cheick Doukoure (Metz/Ufaransa), Franck Kessie (Atalanta Bergamo/Italia), Yao Serge N'Guessan (Nancy/Ufaransa), Jean-Michaël Seri (Nice/Ufaransa)

Washambuliaji: Wilfried Bony (Stoke City/Uingereza), Max-Alain Gradel (Bournemouth/Uingereza), Salomon Kalou (Hertha Berlin/Ujerumani), Jonathan Kodjia (Aston Villa/Uingereza), Nicolas Pepe (Angers/Ufaransa), Giovanni Sio (Rennes/Ufaransa), Wilfried Zaha (Crystal Palace/Uingereza).

Maandalizi
Kikosi cha Ivory Coast kinapiga kambi mjini Abu Dhabi, katika Falme za kiarabu.
Serikali ya Ivory Coast ilitoa Euro Milioni 6 kusaidia maandalizi ya kikosi hiki kutoka Euro 600,000 kama ilivyokuwa miaka miwili iliyopita nchini Equitorial Guinea walikopata ushindi.

Kuelekea katika michuano hii imepangwa kucheza na Uganda na Sweden katika mchuano wa maandalizi.

Timu ya taifa ya Morocco

Kikosi cha Morocco
Kikosi cha Morocco


The Atlas Lions ni timu nyingine katika kundi hili la C.

Mabingwa hawa wa mwaka 1976, wanashiriki katika michuano hii kwa mara 16.

Mara ya mwisho kwa Atlas Lions kushiriki katika michuano hii ilikuwa ni mwaka 2013 nchini Afrika Kusini na kuondolewa katika hatua ya makundi.

Safari ya kwenda Gabon
Morocco ilimaliza wa kwanza la kundi la F kwa alama 16 katika michuano ya kufuzu kwenda nchini Gabon.

Baada ya michuano sita, ilishinda mechi tano nyumbani na ugenini na kwenda sare mchuano mmoja ilipotoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Libya.

Morocco imepangwa katika kundi la C na Togo, Ivory Coast na DRC.

Mwaka 2013, iliondolewa katika hatua ya makundi na inatumai kuwa mwaka huu mambo yatakwenda vizuri.

Kocha
Kocha wa sasa wa Morocco ni Mfaransa, Herve Renard.

Alianza kuifunza timu hiyo mwaka 2016.

Mwaka 2015 akiifunza Cote Dvoire, aliisaidia kushinda taji la AFCON baada ya kusubiri kwa muda mrefu.

Mwaka 2012 akiifunza Zambia, aliiongoza kunyakua taji lake la kwanza wakati michuano hii ilipofanyika nchini Gabon.

Renard mwenye umri wa miaka 28, ambaye anajivunia rekodi nzuri barani Afrika Afrika, mwaka 2010 aliwahi pia kocha wa Angola lakini pia klabu ya USM Alger mwaka 2011 nchini Algeria.

Kikosi

Makipa : Munir Kajoui (Numancia/ESP), Yassine Bounou (Girona/ESP), Yassine Kharroubi (Lokomotiv Plodviv/BUL).

Mabeki: Mehdi Benatia (Juventus/Italia ), Marouane Da Costa (Olympiakos/Ugiriki), Amine Attouchi (Wydad Casablanca), Fouad Chafik (Dijon/Ufaransa), Hamza Mendil (Lille/Ufaransa), Nabil Dirar (Monaco/Ufaransa), Romain Saiss (Wolverhampton/Uingereza).

Viungo wa Kati: Mounir Obbadi (Lille/Ufaransa), Karim El Ahmadi (Feyenoord/Uholanzi), Youssef Ait Bennasser (Nancy/Ufaransa), Mbarek Boussoufa (El Jazira/Falme za Kiarabu, Fayçal Fajr (Deportivo La Corogne/Uhispania), Noureddine Amrabat (Watford/Uingereza), Soufiane Boufal (Southampton/Uingereza), Mehdi Carcela (Granada/Uhispania).

Washambuliaji: Youssef El Arabi (Lekhwiya/Qatar), Youssef Ennesyri (Malaga/Uhispania), Khalid Boutayeb (Strasbourg/Ufaransa), Rachid Alioui (Nimes/Ufaransa), Aziz Bouhaddouz (St Pauli/Ujerumani).

Maandalizi
The Atlas Lions inapiga kambi katika Falme za kiarabu.

Itacheza mechi mbili za Kimataifa dhidi ya Iran na Finland kabla ya kwenda nchini Gabon.

 

 

Togo

Kikosi cha Togo
Kikosi cha Togo


Les Eperviers , au The Sparrow Hawks, inashiriki katika michuano hii kwa mara ya nane.

Mara ya mwisho kucheza katika michuano hii ilikuwa ni mwaka 2013 wakati fainali hii ilipochezwa nchini Afrika Kusini na kufika katika hatua ya robo fainali.

Ilianza kucheza katika michuano hii mwaka 1972.

Safari ya kwenda Gabon
Togo ilikuwa katika kundi moja na Tunisia, Liberia na Djibouti katika michuano ya kufuzu kucheza fainali hii.

Kati ya mechi 6 ilizocheza, ilishinda mechi tatu, kwenda sare mabara mbili na kufungwa mara moja.

Ilifuzu kama mojawapo ya timu bora iliyomaliza katika nafasi ya pili katika michuano hii.
Kocha
Kocha wa Togo ni Mfaransa Claude le Roy.

Le Roy mwenye umri wa miaka 68, ambaye ana historia ya kipekee kufunza soka kwa muda mrefu barani Afrika, alijiunga na Togo mwaka 2016.

Mbali na Togo, amewahi kuwa kocha wa Congo Brazaville kati ya 2013-2015, DR Congo 2011-2013, Ghana 2006-2008, DR Congo 2004-2006, Cameroon 1998, 1985-1988, Senegal 1989-1992.

Kikosi
Makipa: Kossi Agassa (Hana Klabu), Cedric Mensah (Le Mans/Ufaransa), Baba Tchagouni (Marmande/Ufaransa)

Mabeki: Serge Akakpo (Trabzonspor/Uturuki), Vincent Bossou (Young Africans/Tanzania), Djene Dakonam (Saint-Trond/Belgium), Joseph Douhadji (Rivers Utd/Nigeria), Maklibe Kouloun (Dyto), Gafar Mamah (Dacia/MDA), Sadate Ouro-Akoriko (Al Khaleej/KSA), Hakim Ouro-Sama (Port)

Viungo wa Kati: Lalawele Atakora (Helsingborgs/Sweden), Franco Atchou (Dyto), Floyd Ayite (Fulham/Uingereza), Ihlas Bebou (Fortuna Dusseldorf/Ujerumani), Matthieu Dossevi (Standard Liege/Ubelgiji), Henritse Eninful (Doxa/Ujerumani), Serge Gakpe (Genoa/Italia), Victor Nukafu (Entente II), Alaixys Romao (Olympiacos/Ugiriki, Prince Segbefia (Goztepe/Uturuki)

Washambuliaji: Emmanuel Adebayor (Hana klabu, capt), Komlan Agbeniadan (WAFA/Ghana), Razak Boukari (Chateauroux/Ufaransa), Fo Doh Laba(Berkane/Morocco)

Maandalizi
Kikosi cha Togo, kiliwasili nchini Senegal kwa usafiri wa ndege ya rais Faure Gnassingbe, kwa maandalizi ya michuano hii muhimu kabla ya kwenda nchini Gabon.
Togo imepangwa pamoja na Cote d’Ivoire, DR Congo na Morocco.

KUNDI D,
Ghana

Kikosi cha Ghana
Kikosi cha Ghana

Hii ni fainali ya 21 ya Black Stars ya Ghana.

Mara ya mwisho kushiriki katika michuano hii ilikuwa ni mwaka 2015.

Mara ya mwisho kushinda taji hili ilikuwa ni mwaka 1982. Lakini pia imewahi kushinda taji hili mwaka 1963,1965 na 1978.

Mwaka 2015, Ghana ilifika katika hatua ya fainali lakini ikashindwa mbele ya Ivory Coast kwa penalti 9-8 baada ya mchuano huo kumalizika kwa sare ya kutofungana.

Safari ya kwenda Gabon
Ghana ilifuzu katika fainali hii baada ya kushinda mataifa mengine ya Msumbiji, Rwanda na Mauritius.

Kati ya mechi sita ilizocheza, Ghana ilishinda mechi nne, ikatoka sare michuano miwili na hivyo kumaliza kundi hilo kwa ushindi wa alama 14.

Kocha
Mkufunzi wa Black Stars ni Avram Grant raia wa Israeli. Ajipewa kibarua cha kuifunza, Ghana mwaka 2014 baada ya kuchukua nafasi ya Kwesi Appiah.

Grant mwenye umri wa miaka 61, ni miongoni mwa makocha wachache barani Afrika ambao wana uzoefu mkubwa wa kufunza soka.

Kabla ya kuifunza Ghana, aliwahi pia kuifunza nchi yake ya Israel kati ya mwaka 2002-2006.

Mbali na timu za taifa, amewahi pia kufunza vlabu vya Portsmouth, West Ham United na Chelsea ya Uingereza.

Kikosi:
Kocha Grant amekitaja kikosi chake cha mwisho kuelekea nchini Gabon.

Makipa: Razak Braimah (Cordoba, Uhispania), Abdul-Fatau Dauda (Enyimba, Nigeria), Richard Ofori (Wa All Stars)

Mabeki: Harrison Afful (Columbus Crew, Marekani), Andy Yiadom (Barnsley, Uingereza), Baba Rahman (Schalke, Ujerumani), Frank Acheampong (Anderlecht, Ubelgiji), (John Boye (Sivasspor, Uturuki), Jonathan Mensah (Columbus Crew, Marekani), Daniel Amartey (Leicester City, Uingereza), Edwin Gyimah (Orlando Pirates, Afrika Kusini)

Viungo wa Kati: Emmanuel Agyemang-Badu (Udinese, Italia), Afriyie Acquah (Torino, Italia), Thomas Partey (Atletico Madrid, Uhispania)  Mubarak Wakaso (Panathinaikos, Ugiriki), Christian Atsu (Newcastle, Uingereza), Ebenezer Ofori (AIK Stockholm, Sweden), Samuel Tetteh (Leifering, Austria)

Washambuliaji: Asamoah Gyan (Al Ahly, Falme za Kiarabu) Jordan Ayew (Aston Villa, Uingereza), Andre Ayew (West Ham, Uingereza), Ebenezer Assifuah (Sion, Switzerland), Bernard Tekpetey (Schalke, Ujerumani)

Maandalizi

Ghana imekuwa katika maandalizi ya michuano hii mjini Dubai katika nchi ya Falme za kiarabu.

Kikosi hiki kinatarajiwa kuwasili nchini Gabon tarehe 15.

Black Stars, imejumuishwa katika kundi moja na Mali, Misri na Uganda.

Mchuano wa kwanza utakuwa dhidi ya Uganda tarehe 17 dhidi ya Uganda mjini Port-Gentil.

Mali

Kikosi cha Mali
Kikosi cha Mali


Mali inashiriki katika makala ya 10 ya michuano hii. Inafahamika kwa jina maarufu la Les Aigles (The Eagles).

Mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 2015 Equitorial Guinea, lakini ikaondolewa katika hatua ya makundi.

Haijawahi kushinda taji hili lakini mwaka 1972, ilimaliza katika nafasi ya pili katika michuano hiyo.

Safari ya kwenda Gabon.
Mali ilifuzu katika michuano hii baada ya kuongoza kundi la C, kufuzu kwenda nchini Gabon baada ya kumaliza ya kwanza kwa alama 16, mbele ya Benin, Equitorial Guinea na Sudan Kusini.

Kati ya mchezi sita ilizocheza, The Eagles walifanikiwa kupata ushindi katika michuano mitano na kutoka sare mchuano mmoja.

Kocha
Kocha wa Mali ni Mfaransa, Alain Giresse.

Giresse mwenye umri wa miaka 64, aliugana na Mali mwaka 2015, lakini amewahi kuifunza nchi hiyo kati ya mwaka 2010-2012.

Gabon ilikuwa nchi yake ya kwanza kufunza barani Afrika kati ya mwaka 2006-2010 na Senegal kati ya mwaka 2013-2015.

Mbali na timu za taifa, amewahi pia kufunza FAR Rabat ya Moroco kati ya mwaka 2001-2003, Tolouse na Paris Saint-Germain nchini Ufaransa lakini pia kati ya mwaka 2004-2005, aliifunza timu ya taifa ya Georgia.

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Bordeaux na Marseille lakini pia timu ya taifa ya Ufaransa.

Kikosi
Makipa: Soumaila Diakité and Djigui Diarra (Stade Malien de Bamako), Oumar Sissoko (Orléans, Ufaransa)

Mabeki: Ousmane Coulibaly (Panathinaikos, Ugiriki), Hamari Traore (Reims, Ufaransa), Molla Wagué (Udinese, Italia), Salif Coulibaly (TP Mazembe, DR Congo), Mohamed Oumar Konaté (RS Berkane, Morocco), Mahamadou N’Diaye (Troyes, Ufaransa), Youssouf Koné (Lille, Ufaransa)

Viungo wa Kati: Yves Bissouma (Lille, Ufaransa), Mamoutou N’Diaye (Royal Antwerp, Ubelgiji), Lassana Coulibaly (Bastia, Ufaransa), Yacouba Sylla (Montpellier, Ufaransa), Samba Sow (Kayserispor, Uturuki), Adama Traoré (AS Monaco, Ufaransa), Sambou Yatabaré (Werder Bremen, Ujerumani)

Washambuliaji: Moussa Marega (Vitória Guimarães, Ureno), Kalifa Coulibaly (Gent, Ubelgiji), Moustapha Yatabaré (Karabukspor, Uturuki), Bakary Sako (Crystal Palace, Uingereza), Moussa Doumbia (Rostov, Urusi).

Maandalizi
Mali inapiga kambi mjini Casablanca Morocco kabla ya kwenda nchini Gabon.
Imepangwa katika kundi moja na Uganda, Misri na Ghana.

 

Uganda

Kikosi cha Uganda
Kikosi cha Uganda


Uganda Cranes inarejea katika fainali hizi kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1978.
Haya ni mashindano ya 6 kwa Uganda ambayo mara ya wkanza ilishiriki mwaka 1962 na kumaliza wa nne.

Historia ya mwaka 1978 bado inakumbukwa kwa sababu, Uganda ilifika katika hatua ya fainali na Ghana lakini kwa bahati mbaya haikufanikiwa kushinda taji hilo.

Safari ya kwenda Gabon
Uganda ilikuwa katika kundi moja na Burkina Faso, Botswana na Comoros kutafuta nafasi ya kwenda nchini Gabon.

Kati ya mechi sita ilizocheza nyumbani na ugenini, ilishinda mechi nne, ikatoka sare mchuano mmoja na kufungwa mmoja.

Ilimaliza kundi hilo katika nafasi ya pili kwa alama 13, nyuma ya Burkina Faso ambayo pia ilikuwa na alama 13 lakini wingi wa mabao.

Uganda Cranes ilifuzu kama mshindi wa pili wa michuano hiyo ya kufuzu.

Kufuzu kwa Uganda kulileta furaha kubwa sana nchini humo lakini pia katika nchi jirani za Afrika Mashariki, baada ya miaka 38, ya kutafuta tiketi hiyo.

Kocha
Kocha wa Uganda ni Mserbia, Milutin Sredojević maarufu kama Micho.

Micho mwenye umri wa miaka 47, alianza kuifunza Uganda Cranes kuanzia mwaka 2013, baada ya kuchukua nafasi iliyoachwa na Bobby Williamson kutoka Scotaland.

Ameisaidiwa Uganda kushinda taji la kila mwaka la timu bora mwaka 2016, baada ya kuisaidia kufuzu michuano ya AFCON 2017.

Mbali na Uganda, Micho aliwahi kuifunza Rwanda kati ya mwaka 2011-2013.

Ametajwa kuwa miongoni mwa makocha waliofunza soka barani Afrika kwa muda mrefu.

Amewahi kuifunza Sports Club Villa ya Uganda, Saint-George ya Ethiopia, Orlando Pirates, Yanga FC ya Tanzania, Al-Hilal Omdurman ya Sudan.

Kikosi
Makipa: Denis Onyango (Mamelodi Sundowns/Afrika Kusini) , Robert Odongkara (Saint George/Ethiopia) Salim Jamal (AL Merreikh/Sudan)

Mabeki: Joseph Ochaya (KCCA) Timothy Dennis Awany (KCCA) Shafik Batambuze (Tusker/KEN) Dennis Iguma (Al Ahed/Lebanon ) Isaac Isinde (Hana klabu) Murushid Juuko (Simba/Tanzania) Nicholas Wadada (Vipers)

Viungo wa Kati: Tony Mawejje (Throttur/Iceland) Khalid Aucho (Baroka/Afrika Kusini) Luwagga William Kizito (Rio Ave/Ureno) Moses Oloya (Hanoi T and T/VIE) Geoffrey Kizito (Than Quang Ninh/Vietnam) Godfrey Walusimbi (Gor Mahia/Kenya) Hassan Mawanda Wasswa (Nijmeh/Lebanon) Mike Azira (Colorado Rapids/Marekani)

Washambuliaji: Faruku Miya (Standard Liege/Ubelgiji) Geoffrey Massa (Baroka/Afrika Kusini) Muhammad Shaban (Onduparaka) Yunus Sentamu (Ilves/Finland), Geoffrey Sserunkuma (KCCA).

Maandalizi
Uganda inapiga kambi mjini Dubai katika Mmiliki za kiarabu. Mchuano wa kirafiki dhidi ya Tunisia na Ivory Coast.

Imepangwa pamoja na Ghana, Misri na Togo.

Misri

Kikosi cha Misri
Kikosi cha Misri

Haya yatakuwa mashindano ya 23 kwa timu ya taifa ya Misri.

Misri inayofahamika kama Pharaohs, wanarejea katika michuano hii kwa mara ya kwanza baada ya kushiriki mara ya mwisho mwaka 2010.

Inasalia kuwa taifa bora, kuweka historia ya kushinda mataji mengi ya taji hili, mara 7 mwaka 1957,1959,1986,1998,2006,2008 na 2010.

Safari ya kwenda Gabon
Misri ilipangwa katika kundi moja na Nigeria na Tanzania katika michuano ya kufuzu kwa fainali ya mwaka huu.

Kati ya mechi nne ilizocheza nyumbani na ugenini baada ya Chad kuondolewa katika michuano hiyo, ilishinda mechi tatu na kutoka sare mchuano mwingine na hivyo kuongoza kundi la G kwa alama 10.

Hali ya kisiasa imekuwa ikielezwa kuwa moja ya sababu ya Misri kukosa kufika katika michuano hii tangu mwaka 2010, na kuwepo kwao huenda kukaleta ladha tofauti.

Kocha.
Kocha wa timu hii ni raia wa Argetina Héctor Cúper.

Cúper mwenye umri wa miaka 61, alianza kuifunza Misri mwaka 2015.

Misri ndio timu ya kwanza ya taifa kufunzwa na kocha huyu ambaye ana uzoefu mkubwa kufuza soka katika vlabu mbalimbali.

Alianza kufunza soka mwaka 1993, wakati huo akiifunza klabu ya Huracan.
Aidha, amewahi kuifunza Internationale ya Italia kati ya mwaka 2001-2003, Mallorca 2004-2006 na Parma mwaka 2008.

Kabla ya kupewa kibarua nchini Misri, alikuwa anaifunza Al Wasl FC kutoka Falme za Kiarabu kati ya mwaka 2013-2014.

Kikosi
Makipa: Ahmed El-Shennawy (Zamalek), Essam El-Hadary (Wadi Degla), Sherif Ekramy (Al Ahly)  

Mabeki: Ahmed Fathi (Al Ahly), Ahmed Elmohamady (Hull City – Uingereza), Mohamed Abdel-Shafy (Al-Ahli – Ksa), Karim Hafez (Lens – Ufaransa), Ahmed Hegazy (Al Ahly), Saad Samir (Al Ahly), Ahmed Dweidar (Zamalek), Ali Gabr (Zamalek), Omar Gaber (Basel – Uswizi).

Viungo wa Kati: Mohamed Elneny (Arsenal – Uingereza), Tarek Hamed (Zamalek), Ibrahim Salah (Zamalek), Abdallah El-Said (Al Ahly), Amr Warda (Panetolikos – Ugiriki), Ramadan Sobhi (Stoke City – Uingereza), Mahmoud Hassan ‘Trezeguet’ (Royal Mouscron – Ubelgiji).  

Washambuliaji: Ahmed Hassan ‘Koka’ (Braga – Ureno), Marwan Mohsen (Al Ahly), Mahmoud Abdel-Moneim ‘Kahraba’ (Al-Ittihad – Ksa), Mohamed Salah (As Roma – Italia).

Maandalizi
Misri ambayo ipo katika kundi D na Ghana, Mali na Ghana. Itacheza michezo yake ya makundi katika mji wa Port Gentil.

Misri ambao wamekuwa wakifanya mazoezi yao mjini Cairo, watamenyana na Mali katika mchuano wao wa ufunguzi tarehe 17.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.