Pata taarifa kuu
SOKA-DROGBA-MONTREAL

Drogba mbioni kuachana na klabu ya Montreal

Mchezaji nyota wa Cote d'Ivoire Didier Drogba amewathibitishia waandishi wa habari kwamba ataachana na klabu ya Montreal ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Didier Drogba dhidi ya klabu ya Philadelphia Union, Agosti 22, 2015 mjini Montreal.
Didier Drogba dhidi ya klabu ya Philadelphia Union, Agosti 22, 2015 mjini Montreal. © Graham Hughes/AP/SIPA
Matangazo ya kibiashara

"Ni mechi yangu ya mwisho hapa," Didier Drogba amewambia waandishi wa habari baada ya mcechi ya wali ya nusu fainali ya ligi ya Amerika ya Kaskazini (MLS) ambapo Montreal walishinda mabao 3-2 dhidi ya Toronto Jumanne Novemba 22.

"Lakini muhimu zaidi, siyo ushindi huu, ni mechi ya marudiano ya nusu fainali, ambayo tunapaswa kupata ushindi," ameongeza didier Drogba ambaye aliingia uwanjani katika dakika ya ishirini ya kabla ya kumalizika kwa mchuano huo.

Mara tu baada ya meci hii ya awali ya nusu fainali, Montreal ilieandaa sherehe ya kumuaga Didier Drogba katika uwanja wa Olimpiki. Katika sherehe hiyo, dier Drogba alipewa zaiwadi nono ili kuonyesha kuwa klabu ya Montreal itamkumbuka sana. Mshambuliaji huyu wa zamani wa Chelsea, mwenye umri wa miaka 38, alichukua nafasi ya kuwashukuru mashabiki wa klabu ya Montreal na viongozi wake.

"Nimetaka kuishukuru klabu ya Montreal kwa kuwa na imani na mimi, hii ilikua moja ya ndoto zangu, hapa ni mahali ambapo nilitaka kuwa, nawashukuru nyote kutoka moyoni mwangu," Bw Drogba alisema. "Tuliishi vizuri pamoja, tulifurahi pamoja, ni jambo la kusikitisha kuona hali hii haitorudi ten apamoja nanyi," ameongeza Didier Drogba ambaye ataendelea kusakata kabumbu katika klabu mpya, angalau hadi mwisho wa msimu 2017- 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.