Pata taarifa kuu
FIFA-UINGEREZA-SCOTLAND

Fifa yazionya Uingereza na Scotland ikiwa watakaidi maelekezo yake

Katibu mkuu wa shirikisho la soka duniani FIFA, Samba Diouf Samoura, ameionya nchi ya Uingereza na Scotland kuwa huenda zikakabiliwa na adhabu ikiwa timu zao zitavaa kitambaa maalumu chenye alama ya ua jekundu "Poppies" katika mchezo wao wa Novemba 11.

Waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May akivaa "Poppies" baada ya kununua, Fifa imepiga marufuku ua hili kuwekwa kwenye jezi za timu ya taifa, London, October 31, 2016.
Waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May akivaa "Poppies" baada ya kununua, Fifa imepiga marufuku ua hili kuwekwa kwenye jezi za timu ya taifa, London, October 31, 2016. REUTERS/Stefan Wermuth
Matangazo ya kibiashara

Juma hili chama cha soka cha Uingereza na kile cha Scotland, viliapa kukaidi maelekezo ya FIFA, ambayo yanazuia wachezaji kuvaa vitambaa au jezi zenye matangazo ya biashara, siasa au ishara za kidini wakati wa mechi.

Wananchi wa Uingereza huvaa vitambaa vyenye kiua kinachofahamika kama "Poppies" kuwakumbuka watu waliopoteza maisha kwenye vita, ambapo chama cha soka cha Uingereza kimesema kuwa itakuwa ni vyema zaidi ikiwa wachezaji hao watavaa vitambaa vyeusi vyenye kiua chekundu kuadhimisha siku hii.

Akizungumza na shirika la habari la Uingereza, katibu mkuu Samoura amesema kuwa "lazima tuwe na msimamo ulio sawa kwa nchi zote wanachama 211 kwa kuheshimu sheria za mchezo.

"Uingereza sio nchi pekee duniani ambayo imeathirika kutokana na vita. Swali ni kwamba kwanini wao sasa wanataka kulifanya suala lao kuwa la kipekee duniani?"

Uingereza itacheza na Scotland Novemba 11 kwenye mchezo wa kufuzu kusaka tiketi ya kucheza fainali ya kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi, mchezo ambao umepangwa kufanyika siku ambayo Uingereza huadhimisha kumbukumbu ya watu waliokufa kwenye vita.

Alipoulizwa ikiwa kuna uwezekano wa timu hizo kuchukuliwa hatua ikiwa zitakaidia maagizo yake, katibu mkuu Samoura amesema kuwa "Sio nia yangu kumuhukumu mtu yeyote.

"Wanapaswa kufahamu kuwa wao wenyewe ni sehemu ya sheria za mchezo na wanatakiwa kuwa tayari kukabiliwa na adhabu yoyote wakikaidi."

Juma hili pia, waziri mkuu wa Uingereza Theresa May alisema uamuzi wa FIFA "unachukiza".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.