Pata taarifa kuu
FIFA-SOKA-UFISADI

Kiongozi mmoja Afrika Kusini alengwa na FIFA

Kamati ya maadili ya Shirikisho la kimataifa la Soka (FIFA) limeomba kusimamishwa kwa angalau miaka sita dhidi ya rais wa zamani wa Shirikisho la Soka la Afrika Kusini, Kirsten Nematandani.

Nembo ya Shirikisho la kimataifa la Soka (FIFA) mbele ya shirikisho hilo mjini Zuric Oktoba 8, 2015.
Nembo ya Shirikisho la kimataifa la Soka (FIFA) mbele ya shirikisho hilo mjini Zuric Oktoba 8, 2015. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Kamati ya Maadili ya FIFA inamshtumu kukiuka sheria zinazosimamia mpangilio wa mechi za kimataifa za kirafiki nchini Afrika Kusini mwaka 2010.

Miaka minne iliyopita,Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) lilimsimamisha Kirsten Nematandani, likisema kuwa na ushahidi kwamba alishiriki katika ukiukaji wa sheria na kuzipa ushindi baadhi ya timu baada ya kupewa hongo.

Wachunguzi wanakumbusha kwamba wamekuwa wamependekeza mjumbe wa zamani wa Kamati ya Uongozi ya Shirikisho la Soka la Zimbabwe, Jonathan Musavengana, asimamishwe maisha, na kocha wa zamani wa Togo, Tchanile Banna, kwa madai ya rushwa.

Uamuzi wa mwisho juu ya viongozi hawa watatu utachukuliwa na jopo la majaji wa FIFA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.