Pata taarifa kuu
MICHEZO-ETO'O-SOKA

Eto'o asimamishwa na klabu yake

Klabu ya Uturuki ya Antalyaspor imemsimamisha kushiriki michuano mshambuliaji wa Cameroon Samuel Eto'o hadi utakapotangazwa tena uamuzi mwengine, ikimtuhumu kutoa kauli za ubaguzi wa rangi kwenye mitandao ya kijamii.

Samuel Eto'o akabiliwa na kibarua kigumu katika klabu yake ya Antalyaspor.
Samuel Eto'o akabiliwa na kibarua kigumu katika klabu yake ya Antalyaspor. Getty Images
Matangazo ya kibiashara

"Labda baadhi ya watu hawaniheshimu kwa sababu mimi ni mweusi, " ameandika nahodha wa zamani wa Simba wa Nyika kwenye akaunti yake ya Instagram.

Eto'o hakusema ni nani aliyekua akimzungumza kwa kumwandikia maneno hayo, wiki chache baada ya kiongozi wa klabu ya Antalyaspor, Safak Ali Ozturk, alipoonekana akimkosoa mshambulizi huyo wa Cameroon, mwenye umri wa miaka 35 kwa ajili ya utendaji wake.

"Hakuna mchezaji aliye juu ya maslahi ya klabu yaAntalyaspor. Kila mtu anapaswa kujua nafasi yake, " alisema Bw Ali, kauli iliyomlenga Samuel Eto'o.

Kwa mujibu wa baadhi vyombo vya habari vya Uturuki, maoni ya Samuel Eto'o kwenye Instagram yanamlenga Safak Ali Ozturk, lakini mshambuliaji huyo aliruha ujumbe mwingine kwenye mtandao huo wa kijamii, akisema hakumlenga kiongozi wa klabu yake.

Klabu ya sasa ya mchezaji wa zamani wa FC Barcelona, wa Inter Milan na Chelsea iko katika hali ngumu katika msimu huu. Ina alama moja kwa jumla ya mechi nne ambazo imecheza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.