Pata taarifa kuu
CAMEROON-HUGO-SOKA

Cameroon: Hugo Broos kocha mpya wa Simba wa Nyika

Shirikisho la Soka nchini Cameroon (FECAFOOT) limemkabidhi Hugo Broos, raia wa Ubelgiji timu ya taifa ya Cameroon, kwa kuweza kuinoa.

Hugo Broos, raia wa Ubelgiji.
Hugo Broos, raia wa Ubelgiji. AFP / BELGA / PETER DECONINCK -- BELGIUM OUT --
Matangazo ya kibiashara

Kocha huyu, mwenye umri wa miaka wa 63 hakua amepewa nafasi kubwa ya kumrithi Mjerumani, Volker Finke, kwa nafasi ya kuwanoa Simba wa Nyika.

Alain Giresse, Claude Le Roy Hervé Renard wote raia wa Ufaransa, ni miongoni mwa majina ambayo yalipewa nafasi kubwa ya kuchukua na fasi ya Volker Finke. Lakini hadi dakika ya mwisho wamejikuta wamepigwa mweleka na Hugo Broos, raia wa Ubelgiji, ambaye hakuwa amepewa nafasi kubwa ya kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Cameroon. Shirikisho la Soka nchini Cameroon (FECAFOOT) limeamua kumkabidhi nafasi ya Volker Finke raia wa Ubelgiji, Hugo Broos.

Hugo Broos, kocha mwenye umri wa miaka 63, ambaye aliongoza klabu kadhaa za Ubelgiji (FC Bruges, Excelsior Mouscron, Anderlecht, Genk Zulte Waregem), Ugiriki, Uturuki, UMoja wa Falme za Kiarabu, vilevile nchini Algeria.

Hugo Broos, beki wa zamani wa Red Devils, aliinoa klabu ya JS Kabylie mwaka 2014 na kisha klabu ya NA Hussein Dey.

Hugo Broos aanza na michuano ya mtoani ya AFCON Machi 26

Sven Vandenbroeck, raia wa Ubelgiji na Mcameroon Alexandre Belinga, ambaye alikua akihudumu kama kaimu kocha katika miezi ya hivi karibuni, watakuwa wasaidizi wa Hugo Broos. Chaguo hilo limefanywa Februari 12, 2016 na rais wa FECAFOOT, Roko Tombi Sidiki

Hugo Broos anatarajiwa kufanya vizuri Machi 26 katika uwanja wa Limbe, dhidi ya Afrika Kusini, katika michuano ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017). Kazi kubwa inayomsubiri ni kufuzu kwa Cameroon kwa michuano ya Kombe la Matiafa ya Afrika 2017 na michuano ya Kombe la Dunia 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.