Cristiano Ronaldo aionya klabu yake ya Real Madrid licha ya kupata ushindi
Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Real Madrid kutoka nchini Uhispania Cristiano Ronaldo, ameonya kuwa huenda timu yake ikaadhibiwa vikali katika siku zijazo ikiwa haitabadilika katika michuano inayoendelea ya hatua ya makundi kuwania taji la klabu bingwa barani Ulaya UEFA.
Imechapishwa:
Kauli hii ya Ronaldo inakuja baada ya timu yake kuishinda Sporting Lisbon ya Ureno mabao 2-1 Jumatano usiku katika uwanja wao wa nyumbani wa Santiago Bernabeu.
Madrid ambao ni mabingwa watetezi wa taji hili, walijihakikishia ushindi katika dakika za lala salama baada ya Alvaro Morata kutikisa nyavu dakika nne kabla ya kumalizika kwa mchuano huo.
Ronaldo ambaye aliwahi kuichezea Sporting Lisbon akiwa na miaka 12, alikataa kusherehekea goli alilofunga, na badala yake kuinua mikono yake kuonesha ishara ya kuomba radhi kwa mashabiki wa klabu yake ya zamani.
Matokeo mengine ya Jumatano usiku Septemba 14 2016:-
- Manchester City 4-0 Borussia Monchengladbach
- Bayer Leverkusen 2-2 CSKA Moskva
- Tottenham Hotspur 1-2 Monaco
- Real Madrid 2-1 Sporting CP
- Legis Warszawa 0-6 Borussia Dortmund
- Club Brugge 0-3 Leicester City
- Porto 1-1 Kobenhavn
- Olympique Lyonnais 3-0 Dinamp Zagreb
- Juventus 0-0 Sevilla
Katika hatua nyingine, michuano ya hatua ya makundi kuwania taji la Europa League inaanza kutifua vumbi Alhamisi usiku.
Ratiba Septemba 15 2016:-
- Nice vs Schalke 04
- PAOK vs Fiorentina
- Sporting Braga vs Gent
- Southmptom vs Sparta Praha
- Villarreal vs Zurich
- Panathinaikos vs Ajax
- Fayenoord vs Manchester United
- Villarreal vs Zurich