Pata taarifa kuu
DRC-AS VITA CLUB-SOKA

AS Vita Club yawakatisha tamaa mashambiki wake

Mashabiki wa klabu ya AS Vita Club wamekasirishwa na hatua ya klabu yao kuondolewa katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika katika dakika za lala salama.

Wachezaji wa klabu ya Congo ya AS Vita Club.
Wachezaji wa klabu ya Congo ya AS Vita Club. AFP PHOTO / JUNIOR D.KANNAH
Matangazo ya kibiashara

Vita club yenye makao yake jijini Kinshasa, iliondolewa siku ya Jumanne kwa kosa la kumchezesha Idrissa Traore aliyekuwa amefungiwa na Shirikisho la soka barani Afrika CAF kucheza mechi nne.

Malalamishi hayo yaliwasilishwa kwa CAF na klabu ya Stade Malien ambayo mchezaji huyo alikuwa anaichezea kabla ya kwenda AS Vita Club.

Traore aliitumikia adhabu ya mchezo mmoja wakati akiichezea Stade Malien, lakini akaichezea klabu ya Mamelodi Sundowns na kuisaidia klabu yake kushinda.

Mchezaji huyo pia aliwahi kuichezea klabu ya Zanzibar, Mafunzo FC, katika hatua ya awali ya michuano hii.

Aidha, ni habari mbaya kwa mchezaji wa kimataifa wa Rwanda Ernest Sugira ambaye hivi karibuni alisajiliwa na klabu hiyo na kuwa na matumaini ya kuonesha ushapavu wake katika michuano hii mikubwa barani Afrika.

Mashabiki wa klabu hii wanahoji inakuwaje kuwa hawakufahamu kuwa mchezaji huyo alikuwa amefungiwa lakini pia inakuwaje, mchezaji mwenyewe alikubali kucheza akiwa anafahamu kuwa amefungiwa kucheza mechi nne?

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.