Pata taarifa kuu
FIFA-KENYA-DRC

CAF yazichulia hatua kali timu za Kenya DRC

Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limeitoza faina ya Dola 10,000 nchi ya Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya mashabiki wa nchi hizo kuvuruga mechi za kufuzu kucheza fainali za mataifa bingwa barani Afrika mwaka ujao nchini Gabon.

Mamlaka ya Tunisia haitaki kuona picha kama hizi zinarudi kutokea katika Uwanja wa Rades. Hapa, ilikua katika fainali kati ya Tunisia na TP Mazembe tarehe 13 Novemba 2010.
Mamlaka ya Tunisia haitaki kuona picha kama hizi zinarudi kutokea katika Uwanja wa Rades. Hapa, ilikua katika fainali kati ya Tunisia na TP Mazembe tarehe 13 Novemba 2010. AFP / FETHI BELAID
Matangazo ya kibiashara

Mashabiki wa Harambee Stars mwezi Machi mwaka huu katika uwanja wa Nyayo, walimzomea mwamuzi na kuanza kurusha chupa za maji uwanjani, baada ya Guinea Bissau kufunga bao.

Kwa mtazamo wa mashabiki wa Kenya na wachezaji wa Harambee Stars, bao lililofungwa halikuwa halali.

Mchuano huo ulisitishwa kwa dakika kadhaa kwa sababu ya vurugu hizo na baadaye kurejelewa huku wageni Guinea Bissau wakiondoka Nairobi kwa ushindi wa bao 1 kwa 0.

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mashabiki wa Leopard nao walijipata katika hali hiyo baada ya Angola kupewa mkwaju wa penalti katika dakika ya tisini ya mchuano huo jijini Kinsasha.

Hatua hiyo iliwakera mashabiki walioamua kuingia uwanjani kwa lengo la kumvamia mwamuzi wa kati na kusitisha upigwaji wa penalti hiyo.

Mchuano huo hata hivyo ulimalizika kwa DRC kupata ushindi wa mabao 2 kwa 1.

Hii sio mara ya kwanza kwa mashabiki wa nchi hizi mbili kujikuta katika hali hii na kupewa adhabu kama hii.

Kanuni za Shirikisho la soka duniani FIFA, lzinampa mamlaka mwamuzi wa katikati kuwa na uamuzi wa mwisho kuhusu mchezo husika na hawezi kusawishiwa na mashabiki wa soka au wachezaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.