Pata taarifa kuu
MAN CITY-REAL MADRID-UEFA

Ligi ya Mabingwa: Manchester City na Real Madrid zatoka sare

Manchester City na Real Madrid ya Zinedine Zidane wametoka sare ya kutofungana (0-0) katika michuano ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Jumanne Aprili 26 katika uwanja wa Etihad Stadium mjini Manchester.

Kipa wa Manchester City akiokoa hatari katika lango lake.
Kipa wa Manchester City akiokoa hatari katika lango lake. Reuters / Phil Noble
Matangazo ya kibiashara

Real Madrid imeshindwa kumpiku hasimu wake wa Uingereza. Cristiano Ronaldo hakucheza mechi hiyo ya jana.

Vijana wa Manuel Pellegrini watamshukuru sana kipa wao Joe Hart,ambaye aliweza kuokoa jahazi katika dakika za mwisho za mchezo huo, na machuano wa marudiano utachezwa katika uwanja wa Santiago Bernabeu. Manchester City imecheza mzunguko wake wa 8 bila kushindwa, wakati ambapo Real, kwa upande wake, imeshindwa kupata ushindi wake wa 10 mfululizo. Hii pia ni mechi ya kumi barani Ulaya ambapo Real Madrid inamaliza bila kufunga bao.

Ronaldo na Benzema wanahitajika

Ingawa klabu ya Madrid klabu inaonekana kuwa na wachezaji bora zaidi kuliko mpinzani wake, inaonekana wazi kwamba itakuwa na haja ya Cristiano Ronaldo na Karim Benzema ndani ya wiki moja ili kuepuka kumuangusha Zidane wakati ambapo katika ligi kuu ya Uhispania (Liga), klabu hii inashikilia nafasi ya 3 nyuma ya Barca na Atletico, ambazo zinaizidi alama moja peke.

Mchuano wa nusu fainali kati ya Real Madrid, ambao wameshinda taji mara kumi, na Machester City, ambao wamefika nusu fainali ya C1 kwa mara ya kwanza katika historia yao, utachezwa Jumatano, Mei 4 mjini Madrid.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.