Pata taarifa kuu
MAN CITY-DYNAMO KIEV-SOKA

UEFA:Dynamo Kiev yaangukia pua kwa kufungwa 3-1 dhidi ya Man City

Manchester city imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Dynamo Kiev katika mchuano uliopigwa Jumatano hii usiku.

Mchezaji kutoka Côte d’Ivoire Yaya Touré (kushoto) Sergio Aguero kutoka Argentina wakati wa ushindi wao wa mabao 3-1 ya Manchester City dhidi ya Dynamo Kiev, Jumanne Februari 24, 2016..
Mchezaji kutoka Côte d’Ivoire Yaya Touré (kushoto) Sergio Aguero kutoka Argentina wakati wa ushindi wao wa mabao 3-1 ya Manchester City dhidi ya Dynamo Kiev, Jumanne Februari 24, 2016.. Reuters / John Sibley Livepic
Matangazo ya kibiashara

Mechi mbili ndio ziliopigwa Jumatano hii usiku: Manchester city ilimenyana na Dynamo Kiev, na Psv Eindhovein wakapimana nguvu na Atletico Madrid.

Mabao mawili ya Manchester City yalifungwa katika kipindi cha kwanza na bao moja likafungwa dakika chache kabla ya kipenga cha mwisho cha mchezo huo.

Mabao ya Manchester city yaliwekwa kimyani na Sergio Aguero katika dakika ya 15 , David Silva katika dakika ya 40, huku bao la tatu likifungwa na Yahya Touré katika dakika ya 90.

Bao la kufutia machozi la Dynamo Kiev lilifungwa na Vital Buyal-sky katika dakika ya 58kipindi cha pili. Dynamo Kiev ilifungwa ikiwa nyumbani.

Katika mechi nyingine Psv Eindhovein wakiwa nyumbani ilitimua vumbi na Atletico Madrid lakini hadi kipenga cha mwisho timu hizi mbili zilijikuta zikitoka sare ya kutofungana.

Michuano hii itaendelea mwezi ujao tarehe 8, 2016. Mechi mbili zitapigwa tarehe hiyo: VfL Wolf- Sburg itamenyana na KAA Gent na Real Madrid itaipokea nyumbani FC Roma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.