Pata taarifa kuu
PSG-AURIER-SOKA

Soka: video ya matusi ya Serge Aurier yazua utata

Mchezaji Serge Aurier anakabiliwa na hali ya sintofahamu kufuatia kurushwa hewani kwa video ambapo alimtusi kocha wake wa Paris Saint-Germain (PSG), Laurent Blanc. Raia huyo wa Cote d'Ivoire pia amewatusi wachezaji wenzake Zlatan Ibrahimovic, Angel Di Maria na Salvatore Sirigu.

Beki wa PSG, Serge Aurier (kulia) akikabiliana na kipa wa Lyon Anthony Lopes katika michuano ya Kombe la Ufarasa (Coupe de France), Februari 10, 2016 katika uwanja wa Parc des Princes.
Beki wa PSG, Serge Aurier (kulia) akikabiliana na kipa wa Lyon Anthony Lopes katika michuano ya Kombe la Ufarasa (Coupe de France), Februari 10, 2016 katika uwanja wa Parc des Princes. FRANCK FIFE/AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Serge Aurier amefutilia mbali madai hayo na kusema kwamba amezushiwa uongo.

Beki huyu wa Paris Saint-Germain (PSG), kwa sasa anakabiliwa na hali ya sintofahamu kutokana na mkanda huo wa video. Mpaka sasa haijafahamika iwapo amezushiwa uongo au amehusika moja kwa moja na tukio hilo.

Serge Aurier, inadaiwa kuwa, alimtukana kocha wake wa PSG, Laurent Blanc, kwamba ni "fieet" [tusi baya linalotumiwa kwa kumaanisha ushoga] na kujibu maswali ya watu wanaotembelea mitandao mbalimbali yaliokua yakiulizwa sauti ya juu na mmoja wa marafiki zake, aliyekuwa naye kwa karibu. Maneno ya matusi yanasikika wakati ambapo winga huyo wa kulia haonekani kabisa katika mhanda huo wa video.

Pia wachezaji wenzake walengwa

Akiketi mbali na Kamera, Serge Aurier alitamka maneno ya kejeli dhidi ya wachezaji wenzake. Akiulizwa kuhusu Angel Di Maria, mwenye umri wa miaka 23, raia wa Argentina Aurier amejibu kuwa mchezaji huyo ni "pembe". Kuhusu kipa bora wa PSG, kati ya Kevin Trapp na Salvatore Sirigu, bingwa wa michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015 amesema "Trapp! Sirigu ni "guez"! (akimaanisha hamna kitu). "

Zlatan Ibrahimovic, mchezaji nyota wa PSG, hakuepuka matusi hayo. Serge Aurier amehakikisha kwamba, raia huyo wa Sweden, hana madaraka juu ya yake: "Zlatan ni mnyama, lakini (usiwi) na wasiwasi na si, ni mnyama mzuri."

Kashfa katika siku mbili za mchuano kati ya PSG na Chelsea

Wachezaji na Klabu ya PSG hawajajibu rasmi kwa saa. Serge Aurier amebaini kwamba amezushiwa uongo wa sauti, kwa mujibu wa mshauri wa runinga ya Canal Plus, Pierre Menes, kabla ya kukiri makosa yake. Srge Aurie hakushiriki mazoezi ya klabu yake ya Jumapili hii Februari 14, na inasadikiwa kuwa hatocheza mechi kati ya klabu yake na Chelsea katika michuano ya Kombe la Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.