Pata taarifa kuu
LIGI YA MABINGWA-SOKA-UEFA

PSG: Thiago Silva, Aurier, Verratti hawatocheza dhidi Shakhtar

Nahodha wa Paris Saint-Germain Thiago Silva atapumzika katika mechi ya mwisho ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Shakhtar Donetsk Jumanne wiki hii, meneja wa PSG, Laurent Blanc, ametangaza, akibaini pia kwamba Marco Verratti na Serge Aurier hawatocheza mechi hiyo.

Beki wa PSG Thiago Silva baada ya mchuano dhidi ya Real Madrid katika michuano ya Ligi ya Mabingwa, Novemba 3, 2015, Bernabeu.
Beki wa PSG Thiago Silva baada ya mchuano dhidi ya Real Madrid katika michuano ya Ligi ya Mabingwa, Novemba 3, 2015, Bernabeu. AFP/AFP/
Matangazo ya kibiashara

Mlinzi wa kati wa Brazil "haitakuwa katika kikosi cha wachezaji 18. Ni uamuzi ambao nimechukua. Alicheza kwa kiasi kikubwa, vizuri sana kwa kweli, kwa hio ameruhusiwa kupumzika, tunamlinda", Laurent Blanc amesema katika mkutano na vyombo vya habari.

Katika kundi la wachezaji 18 walioitishwa, Marco Verratti hayumo. Mchezaji huyo kutoka Italia anauguza jeraha la mguu, lakini "angelipaswa kuwepo" ameeleza Laurent Blanc. Lakini kocha wa PSG ameridhishwa na kutokuwepo kwa mchezaji huyo. "Kwa sasa tuana imani kuwa Marco Verrati atacheza mechi itakayofuata, kwani ana kadi mbili za manjano, iwapo ataonyeshwa kandi nyingine ya manjano, ataondolewa uwanjani na hatocheza mechi ya mzunguko wa nane", amesema Laurent Blanc.

Hali hiyo pia inamkabili Serge Aurier, ambaye pia alionyeshwa kadi mbili za manjano, na iwapo ataonyeshwa kadi nyingine ya manjano, ataukosa mchezo utakaofuata.

Kama ilivyotarajiwa pia, Javier Pastore, anayeuguza jeraha kwa muda mrefu pia hatocheza.

Thiago Motta na Gregory Van Der Wiel, miongoni mwa wachezaji ambao "hawaaminiki" waliotajwa na Laurent Blanc,wako sawa kiafya na stamina.

PSG, ambayo tayari kufuzu katikamzunguko wa nane wa Ligi ya Mabingwa, itaipokea Shakhtar DonetskJumanne hii saa (2:45 usiku), kwa siku ya mwisho ya hatua ya makundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.