Pata taarifa kuu
CHELSEA-SOKA-ULAYA

Guus Hiddink awambia vijana wake kutafakari

Kocha wa mpito wa Chelsea Guus Hiddink amewaambia wachezaji wake kujitazama kwenye kioo na kutia bidii ili kurejesha klabu hiyo katika nafasi yake.

Muhispania Cesc Fabregasna mchezaji kutoka Cote d'Ivoire Didier Drogba (kulia) ni miongoni mwa wachezaji nyota wa Chelsea.
Muhispania Cesc Fabregasna mchezaji kutoka Cote d'Ivoire Didier Drogba (kulia) ni miongoni mwa wachezaji nyota wa Chelsea. Reuters / Toby Melville
Matangazo ya kibiashara

Mholanzi huyo aliyepewa kibarua cha kuifunza the Blues baada ya kufutwa kazi kwa Jose Mourinho kwa sababu ya matokeo mabaya amewaambia wanahabari kuwa anaamini kuwa atakuwa kocha wa klabu hiyo kwa muda mfupi tu.

Hiddink amesema amezungumza na wachezaji wa Chelsea na kujadili wanachohitajika kufanya na pia kugusia hali ilivyokuwa wakati wa kocha Mourihno.

Chelsea inashikilia nafasi ya 15 katika msururu wa ligi kuu kwa alama 18.

The Blues watamenyana dhidi ya Watford siku ya Jumamosi wiki hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.