Pata taarifa kuu
CHELSEA-DYNAMO KIEV-UEFA-SOKA

Jose Mourinho achekelea baada ya ushindi wa klabu yake

Chelsea imeonekana ikitamba uwanjani katika mechi yake dhidi ya Dynamo Kiev katika uwanja wa Stamford Bridge, baada ya kupata ushidi wa mabao 2-1. Ushindi huo wa Chelsea umekua ni gumzo barani ulaya na kwa wapenzi wa soka, baada ya klabu hiyo kushindwa kufanya vizuri katika mechi za Premia.

Meneja wa Chelsea,  Jose Mourinho, amekuwa na masaibu mengi, baada ya klabu yake kuanza vibaya katika michuano ya kutetea taji la Ligi ya Premia.
Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, amekuwa na masaibu mengi, baada ya klabu yake kuanza vibaya katika michuano ya kutetea taji la Ligi ya Premia. REUTERS/Suzanne Plunkett
Matangazo ya kibiashara

Ushindi huu wa Chelsea umepunguza joto kwa mashabiki wa klabu hiyo hasa kwa meneja wake Jose Mourinho ambaye alikua amepoteza imani kwa mashabiki kutokana na kufungwa mara kwa mara kwa klabu hiyo barani Ulaya.

Bao la ushindi wa Chelsea lilifungwa na Willian katika dakika za lala salama, baada ya timu hizi mbili kuwa sare ya bao moja kwa moja.

Mourinho amekuwa na masaibu mengi, baada ya klabu yake kuanza vibaya michuano ya la Ligi ya Premia, ambao klabu yake inashikilia nafasi ya 15.

Ushindi huu wa Chelsea umeifikisha klabu hiyo katika nafasi ya pili katika Kundi G, wakiwa na alama tatu nyuma ya Porto. Hata hivyo bado wana pengo la alama mbili kati yao na Dynamo Kiev.

Itafahamika kwamba familia ya Jose Mourinho, mkewe Matilde, bintiye Matilde Jr na mwanawe wa kiume Jose Jr, walikuwepo uwanjani kumuunga mkono msimamizi wa familia, ambaye ni meneja wa Chelsea. Hata mashabiki wa klabu hiyo wameonekana wakimuunga mkono Jose Mourinho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.