Bayern Munich: Robert Lewandowski aingia katika orodha ya watu waliovunja rekodi
Jumatatu wiki hii, mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski ameingia rasmi katika kitabu cha watu waliovunja rekodi kutokana na kufunga mabao matano dhidi Wolfsburg mwezi Septemba uliyopita, na kumpelekea kuvunja rekodi mara nne.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Hivyo amepata rekodi ya mabao matatu kwa muda mfupi katika historia ya michuano ya Ujerumani(dakika 3 na sekunde 22). Sawa na mabao manne kwa muda wa (dakika 5 na sekunde 42) na vile vile mabao matano kwa muda wa (dakika 8 na sekunde 59). Pia amekua mchezaji wa kwanza katika historia ya Bundesliga kwa kufunga mabao matano baada ya kipindi cha kwanza cha mchezo kuanza akiwa kwenye benchi.
"Ilikuwa usiku wa kihistoria kwangu mimi", mshambuliaji wa kimataifa Poland, mwenye umri wa miaka 27, amesema, wakati akikabidhiwa vyeti vyake vinne. "Ilinichukua muda wa siku kadhaa kutambua, familia yangu ilipigwa na mshangao zaidi kuliko mimi", Robert Lewandowski ameongeza.
Lewandowski, ana mpango wa kutoa jozi ya viatu viliyompelekea kufunga mabao hayo 5 katika hali ya upendo. Tangu kuanza kwa msimu huu amefunga mabao 14.