Maandalizi ya Taifa Stars yakamilika
Nchini Tanzania, maandalizi ya mchezo kati ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Nigeria (Super Eagles) kutafuta nafasi ya kufuzu katika fainali za kombe la Mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017 nchini Gabon yamekamilika.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo huo wa jumamosi katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam huku likiweka kiingilio cha chini kabisa kikiwa shilingi elfu saba .
Wachezaji wa Tanzania ambao walikuwa kambini nchini Uturuki wameendelea kufanya mazoezi jijini Dra es salaam huku wapinzani wao Nigeria wakiwasili leo mchana.
Hta hivyo vijana hao wa Sunday Oliseh wamewasili bila ya kipa wao mahiri Vincent Enyeama baada ya kufiwa na mama yake na sasa nafasi yake itachukuliwa na Carl Ikeme.
Huko nchini Kenya maandalizi ni kama haya ambapo Harambee Stars inajiadaa kupambana na mabingwa wa zamani wa taji hili Chipolopolo ya Zambia siku ya Jumamosi katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.
Tayari kungo wa Kati wa klabu ya Southmton ya Uingereza Victor Wanyama amewasili jijini Nairobi kuungana wenzake pamoja na mchezaji wa zamani Dennis Oliech.
DR Congo nao watakuwa ugenini kumenyana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Uganda nao watakuwa ugenini kumenyana na Comoros, huku Rwanda ikiikaribisha Black Stars ya Ghana.