Pata taarifa kuu
KENYA-SOKA

Kenya: kikosi cha wachezaji 16 wa soka chajulikana

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars Bobby Williamson, amekitaja kikosi cha wachezaji 16 wanaocheza soka nyumbani kuelekea mchuano wa kufuzu kuelekea fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017 dhidi ya Zambia mwezi Septemba.

Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars, ambayo meneja wake ni  Bobby Williamson.
Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars, ambayo meneja wake ni Bobby Williamson. youtube
Matangazo ya kibiashara

Williamson amewataja wachezaji wawili Wycliffe Kasaya na Ian Otieno kujiunga na kikosi hicho cha taifa kutoka katika vlabu vinavyocheza katika daraja la chini.

Kikosi Kamili:

Makipa: Boniface Oluoch (Gor Mahia), Wycliff Kasaya (Nakumatt), Ian Otieno (Posta Rangers).

Mabeki: Harun Shakava (Gor Mahia), Edwin Wafula (AFC Leopards), Dennis Odhiambo (Thika United).

Viungo wa Kati: Collins Okoth (Gor Mahia), Barnard Mang’oli (AFC Leopards), Sammy Meja (Thika United), Humphrey Mieno (Tusker) Eric Johana (Mathare United) Danson Kago (Tusker).

Washambuliaji: Jesse Were (Tusker), Michael Olunga (Gor Mahia), Noah Wafula (Tusker).

Wiki iliyopita, Williamson alikitaka kikosi kingine cha wachezaji 17 wanaocheza soka nje ya nchi.

Kikosi kamili:

-Kipa Arnold Origi – Lillestrom (Norway)

Mabeki: Brian Mandela – Maritzburg United (Afrika Kusini), David Owino – Zesco United (Zambia), David Ochieng (hana timu)

Viungo wa Kati:-Lawrence Olum, Kedah FA (Malaysia), Macdonald Mariga (hana timu), Paul Were (hana timu), Ayub Timbe – SK Lierse (Belgium), Clifton Miheso – VPS FC (Finland), Anthony Akumu – Al Khartoum (Sudan) Victor Wanyama – Southampton FC (Uingereza )

Washambuliaji :- Johanna Omollo – Royal Antwerp FC (Ubelgiji), Dennis Oliech (hana timu), Jacob Kelli –Nkana FC (Zambia), Allan Wanga – Azam FC (Tanzania).
Kenya ilitoka sare ya bao 1 kwa 1 katika mchuano wa ufunguzi wa kundi lao la E dhidi ya Congo Brazaville huku Zambia nao wakitoka sare ya kutofungana na Guinea-Bissau.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.