Pata taarifa kuu
COSAFA

Namibia yanyakua taji la COSAFA

Timu ya taifa ya soka ya Namibia ndio mabingwa wa taji la COSAFA baina ya Mataifa ya Kusini mwa Afrika mwaka huu.

Timu ya taifa ya Namibia
Timu ya taifa ya Namibia
Matangazo ya kibiashara

Brave Warriors, walinyakua taji hilo baada ya kuwashinda Msumbiji mabao 2 kwa 0 katika fainali iliyochezwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa Moruleng nchini Afrika Kusini.

Mabao yote ya Namibia yalitiwa kimyani na Deon Hotto katika kipindi cha kwanza na cha pili cha mtanange huo.

Namibia imepata taji hili kwa mara ya kwanza tangu ilipofika katika hatua ya fainali mwaka 1997 na 1999 huku Msumbiji pia ikifika mwaka 2008.

Nafasi ya tatu ya michuano hiyo ilichukuliwa na Madagascar baada ya kuishinda Bostwana kwa mabao 2 kwa 1.

Mfungaji wa Madagascar alikuwa ni Sarivahy Vombola ambaye pia alimaliza michuano hiyo akiwa mfugaji bora akiwa na mabao matano.

Mechi 23 zilichezwa katika michuano hiyo huku mabao 46 yakifungwa.
Timu ya Tanzania na Ghana zilialikwa katika michuano hiyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.