Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Scolari: Sina shaka timu yangu itatwaa kombe la dunia mwaka huu

Licha ya shinikizo toka kwa mashabiki wa timu ya taifa ya Brazil, kutaka kuona timu hiyo inatwaa taji hilo kubwa zaidi duniani, kocha mkuu wa timu hiyo mkongwe, Luiz Felipe Scolar ameonesha kutokuwa na hofu juu ya hilo.

Kocha wa timu ya taifa ya Brazil, Luiz Felipe Scolari
Kocha wa timu ya taifa ya Brazil, Luiz Felipe Scolari fifa.com
Matangazo ya kibiashara

Mashabiki wa soka nchini Brazil wanataka kuona timu yao ikirejea kwenye fainali za mwaka huu kwa kishindo kwakuwa ndio nchi mwenyeji wa mashindano ya mwaka huu, kwahivyo wanaona ni muhimu wa timu yao kujituma kutwaa taji hili la kombe la fifa.

Scolari mwenye umri wa miaka 65 hivi sasa amewaambia mashabiki wa soka nchini humo kuwa lengo lake ni kutaka kumaliza ukame wa miaka 12 kwa timu hiyo kushindwa kutwaa taji la kombe la dunia la fifa.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Brazil wakishangilia moja ya goli walilofunga
Wachezaji wa timu ya taifa ya Brazil wakishangilia moja ya goli walilofunga fifa.com

Kocha huyu mkongwe amesema kuwa kadri siku zinavyozidi kusogea kufikia kuanza kwa fainali za mwaka huu, anaona kabisa na anakuwa na imani kuwa kikosi chake kiko imara na kwamba kombe litabaki nchini Brazil.

Scolari anasema kuwa "Najua lazima tuheshimu timu nyingine ambazo zinakuja kushiriki kwenye fainali za mwaka huu, lakini niwe muwazi ya kuwa timu yetu ni bora zaidi kwa mwaka huu", anasema Felipe Scolari.

Felipao kama anavyofahamika zaidi nchini mwake Brazil, alirejea kukinoa kikosi cha timu ya taifa December mwaka 2012 baada ya kuwa ameinoa timu ya taifa ya Ureno kwa zaidi ya miaka 5 na wakati fulani kuwa kocha wa timu ya Chelsea ya nchini Uingereza.

Wachezaji wa zamani waliowahi kucheza kwenye timu ya taifa ya Brazil, wanasema kuwa Scolari kwa sehemu kubwa amefanikiwa kuwaunganisha wachezaji wake na wanacheza kitimu zaidi ukilinganisha na miaka kadhaa iliyopita.

Mwaka jana licha ya kupata upinzani mkali wakati wa mechi za kombe la mabara, Brazil ilienda kushinda mechi zake zote tano kabla ya kuwachabanga mabao 3-0 mabingwa watetezi Uhispania kwenye fainali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.