Pata taarifa kuu
BREZIL-Kombe la dunia

Seleçao ya Brazili inapewa matumaini ya kutwaa kombe la dunia

Zico, mchezaji nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil, ambaye alipata umaarufu sana kwa kuvalia jezi nambari 10 mgongoni, anaipa matumaini timu yake ya zamani dhidi ya timu ya taifa ya Argentina katika michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2014, akibaini kwamba Seleçao itatwaa kombe la dunia. Hayo ameyafahamisha katika mahojiano na shirika la habari la AFP.

Picha ya zamani ya Zico, mchezaji nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil katika miaka ya 1978, 1982 na 1986
Picha ya zamani ya Zico, mchezaji nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil katika miaka ya 1978, 1982 na 1986 RFI
Matangazo ya kibiashara

Mshambuliaji huyo wazamani wa Seleçao, mwenenye umri wa miaka 60, ameelezea masikitiko yake, akisema kwamba Brazil imekua na kasumba ya kutoipa kipau mbele sekta ya utalii, mbayo ni miongoni mwa sekta muhimu inayokuza uchumi nchini.

Akihojiwa kuhusu ubora wa timu ya taifa ya Brazil, Zico, amesema kocha wa Seleçao, Felipao Scolari na Carlos Alberto Parreira, ambae ni mrasibu wa timu hio wamefanya vizuri kwa kurejesha uiyano kati ya mashabiki na wachezaji.

Amebaini kwamba Seleçao iltwaa kombe la shirikisho, hali hio ilipelekea kunakuweko na maridhiano baina ya mashabiki na timu hio imewnipa matumaini kuwa Seleçao itatwaa kombe la dunia.

Ni jambo la kawaida, kuwa na motisha iwapo unajezea nymbani. Ufaransa, Argentina, Uingereza, Ujerumani na itali walitwaa kombe la dunia wakiwa nyumbani.

Kulikoni kwa timu ya taifa ya Brazili isifanyi vizuri ikiwa nyumbani, amesema Zico.

Zico amebani kwamba Argentine ndie mpinzani mkuu pekee wa Brazil, kutokana na mchezaji nyota wa timu hio Lionel Messi, ambaye kwa muda wowote anaweza kuipatia ushindi timu yake.

Zico amesema katika enzi zake timu ya Brazil ilikua katika kiwango bora cha mchezo na katika enzi za Ronaldinho na Ronaldo miaka ya 2002, akibaini kwamba hata katika enzi za Roberto Carlos, Rivaldo,.... timu hio iliendelea kuonyesha mchezo mzuri.

“Wakati huu Seleçao haioneshi mchezo mzuri, hata kama kuna baadhi ya wachezaji kama vile Neymar, Oscar, Fred, Thiago Silva, Marcelo, Dani Alves..., ambao wanacheza vizuri, kuna hata wengine , ambao ni wafungaji wazuri”, amesema Zico.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.