Pata taarifa kuu

Israeli/Hamas: Mazungumzo ya kusitisha vita yanaendelea jijini Cairo

Nairobi – Wasuluhishi wa mzozo kati ya Israeli na kundi la Hamas kwenye ukanda wa Gaza, wameendelea na majadiliano jijini Cairo kupata mkataba wa kusitisha vita vinavyoendelea.

Jeshi la angaa la Israeli pia linasema limeshambulia ngome za kundi la Hezbollah, ambalo ni washirika wa karibu wa Hamas  Kusini mwa Lebanon
Jeshi la angaa la Israeli pia linasema limeshambulia ngome za kundi la Hezbollah, ambalo ni washirika wa karibu wa Hamas  Kusini mwa Lebanon REUTERS - Mohammed Salem
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo yanayosimamiwa na Misri, Qatar na Marekani yamerejelewa tena wakati huu jeshi la Israeli likiendeleza mashambulio kwa saa 24 zilizopita, ambayo yamesababisha vofo vya watu 124.

Hata hivyo, ripoti zinasema siku ya Jumatatu, wasuluhushi hao wamekutana na mwakilishi wa kutoka kundi la Hamas, lakini sio wajumbe wa Israeli.

Rais wa Marekani Joe Biden, amesema mara kadhaa kuwa, mkataba wa kusitisha vita unatarajiwa kupatikana kufikia Machi 10 au 11 wakati wa kuanza kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Wakati hayo yakijiri, Jeshi la angaa la Israeli linasema limeshambulia ngome za kundi la Hezbollah, ambalo ni washirika wa karibu wa Hamas  Kusini mwa Lebanon.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya Haki za Binadamu Volker Turk amesema iwapo suluhu haitapatikana haraka, kuna uwezekano mkubwa wa vita vinavyoendelea kusambaa kwenye nchi nyingine za Mashariki ya Kati hasa Yemen na Lebabon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.