Pata taarifa kuu

Gaza: Mashambulio mapya dhidi ya Rafah, mazungumzo magumu kwa ajili ya kusitisha mapigano

Wakati mazungumzo yakianza mjini Cairo kwa ajili ya kusitisha mapigano huko Gaza, Israel imeanzisha mashambulizi mapya ya anga dhidi ya Rafah usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi, na kuua karibu watu 100, kulingana na Hamas. “Hali inazidi kuwa mbaya zaidi,” linaonya Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka, RSF.

Des Palestiniens vérifient les décombres de la mosquée al-Faruq le 22 février 2024, à la suite d'une frappe aérienne israélienne nocturne dans le camp de réfugiés de Rafah, dans le sud de la bande de
Wapalestina wakiangalia vifusi vya msikiti wa al-Faruq mnamo Februari 22, 2024, kufuatia shambulio la anga la usiku la Israel katika kambi ya wakimbizi ya Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza. AFP - SAID KHATIB
Matangazo ya kibiashara

Mjumbe maalum wa Marekani anatarajiwa nchini Israel leo Alhamisi kujaribu kuzindua upya majadiliano kati ya wahusika wakuu tofauti. Lengo? kupata suluhu kwa eneo la Palestina linalokumbwa na milipuko ya kila siku.

Tangu Oktoba 7 na shambulio la Hamas dhidi ya Israeli, operesheni ya kijeshi ya Israeli, ya anga na ya ardhini, imesababisha mzozo mbaya wa kibinadamu. Takriban watu 30,000 wameuawa huko Gaza tangu Oktoba 7, 2023, kulingana na Hamas, na Umoja wa Mataifa umeonya kuwa watu milioni 2.2 wako katika hatari ya njaa.

Wakati wa usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi, mashambulizi mengi yameripotiwa tena katika mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza. Jeshi la anga la Israel lilifanya takriban mashambulizi kumi, kulingana na shirika la habari la AFP. Na kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Hamas, watu 99 waliuawa jana usiku.

"Kuna uharaka wa kukomesha vita hivi"

Licha ya udharura wa hali hiyo kwa idadi ya raia wa eneo la Palestina, mazungumzo yameshindwa kufikia muafaka. "Tunataka makubaliano yafikiwe (...) haraka iwezekanavyo," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Matthew Miller amewaambia wanahabari. Hivi sasa kwenye meza, rasimu ya makubaliano inahusu usitishaji wa mapigano wa wiki sita, unaohusishwa na kubadilishana mateka kwa wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa na Israel na kuingia Gaza kwa kiasi kikubwa cha misaada ya kibinadamu.

Lakini wengine wanaonya juu ya kujikokota kwa mazungumzo ikilinganishwa na uzito wa hali. "Muda wa mazungumzo, wa majadiliano katika ngazi ya Umoja wa Mataifa kati ya serikali si ule unaoshuhudiwa katika Ukanda wa Gaza hata kidogo," anasema Guillemette Thomas, mratibu wa matibabu wa ujumbe wa Palestina wa shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) kutoka Ufaransa. "Nadhani serikali hazielewi maafa yanayotokea leo huko Gaza. Kuna udharura wa kufanya jambo, udharura wa kukomesha vita hivi, udharura wa kukomesha mauaji haya katika Ukanda wa Gaza,” anahimiza.

Na kuongeza: "Maadamu hakuna usitishaji vita wa mara moja na idadi kubwa ya misaada ya kibinadamu, haya ni maneno tu na ukweli wa msingi unamaanisha kuwa tuna ugumu wa kuamini yote hayo." Kwa mujibu wa ripoti ya hivi punde ya Hamas, watu 29,410 wameuawa  katika Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa vita.

(Na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.