Pata taarifa kuu

Gaza: Marekani yapiga kura ya turufu kupinga kusitisha mapigano tena

Hali ya Gaza kwa mara nyingine ilikuwa kiini cha mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne, Februari 20, ambao ulikuwa wa kujadili azimio la kutaka kusitishwa mara moja kwa mapigano. Nakala hiyo ilizuiwa na Marekani.

Nchi 13 za baraza hilo lenye wanachama 15 ziliunga mkono azimio la Algeria, huku Uingereza ikisusia.
Nchi 13 za baraza hilo lenye wanachama 15 ziliunga mkono azimio la Algeria, huku Uingereza ikisusia. AP - Seth Wenig
Matangazo ya kibiashara

 

Rasimu ya azimio hilo, lililotaka "kusitishwa mara moja kwa mapigano ambayo ilipaswa kuheshimishwa na pande zote", ilipata kura kumi na tatu za ndio, moja ya haikuonyesha msimamo wake (Uingereza) na moja ya Marekani imepinga. Hii ni kura ya tatu ya turufu ya Marekani tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na Hamas.

Ikiletwa na kundi la nchi za Kiarabu zinazoongozwa na Algeria baada ya majadiliano ya zaidi ya wiki tatu, nakala hiyo pia inapinga "kulazimishwa kwa raia wa Palestina kuondoka katika maeneo yao", wakati Israeli ilizungumza juu ya kuhamishwa kwa raia kabla ya mashambulizi yake huko Rafah ambapo watu milioni 1.4 wamejazana kusini mwa Ukanda wa Gaza. "Kura kwa rasimu ya azimio hili ni kuunga mkono haki ya kuishi ya Wapalestina. Kinyume chake, kupiga kura dhidi yake kunamaanisha kuunga mkono ghasia za kikatili na adhabu ya pamoja waliyopewa,” amesema Balozi wa Algeria, Amar Bendjama kabla tu ya kupiga kura.

Kama azimio ya hapo awali lililokashifiwa na Israeli na Marekani, nakala hii haikulaani shambulio ambalo lilifanywa na Hamas mnamo Oktoba 7 dhidi ya Israeli. Marekani ilionya wikendi hii kwamba nakala ya Algeria haikubaliki. "Ninaelewa nia ya Baraza la kuchukua hatua haraka (...) lakini nia hii haiwezi kutufanya tusione uhalisia, na haiwezi kudhoofisha njia pekee, narudia, njia pekee inayoongoza kwenye amani ya kudumu," Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield amesema siku ya Jumanne. Mfuasi mkuu wa Israel, Marekani inabaini kwamba azimio hili lingehatarisha mazungumzo ya kidiplomasia ya msingi ili kupata suluhu ikiwa ni pamoja na kuachiliwa tena kwa mateka.

Balozi wa Washington katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield, amesema sio wakati mwafaka wa kutaka kusitishwa kwa mapigano mara moja huku mazungumzo kati ya Hamas na Israel yakiendelea.

Hapo awali Marekani iliepuka neno "kusitisha mapigano" wakati wa kura za Umoja wa Mataifa kuhusu vita hivyo, lakini Rais Joe Biden hivi karibuni ametoa maoni kama hayo.

Mswada wa azimio uliopendekezwa na Marekani unatoa wito wa kusitishwa kwa mapigano kwa muda "haraka iwezekanavyo" na kwa sharti kwamba mateka wote waachiliwe, pamoja na kutaka vizuizi vya misaada kufikia Gaza viondolewe.

Hata hivyo, haijulikani ikiwa au lini Baraza la Usalama litapiga kura kwa njia ya maneno yaliyopendekezwa na Washington.

(Na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.