Pata taarifa kuu

Hamas yataka kusitishwa kwa mapigano na Israel iondoke Gaza

Kiongozi wa kundi la wanamgambo kutoka Palestina la Hamas Ismail Haniyeh amekariri siku ya Jumamosi kwamba vuguvugu lake linata kusitishwa kwa mapigano na Israel iondoke katika Ukanda wa Gaza, kama sehemu ya mazungumzo yanayoendelea kwa ajili ya usitishwaji mapigano.

Katika picha hii iliyotolewa na serikali ya Lebanon, Ismail Haniyeh, kiongozi wa kundi la wapiganaji wa Palestina la Hamas, akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya kukutana na Rais wa Lebanon Michel Aoun, katika ikulu ya rais, huko Baabda, mashariki mwa Beirut, Lebanon, Jumatatu, Juni. 28, 2021. Hamas ilisema Jumatano, Desemba 20. 2023, kiongozi wake mkuu, Ismail Haniyeh, amewasili Cairo kwa mazungumzo kuhusu vita huko Gaza.
Katika picha hii iliyotolewa na serikali ya Lebanon, Ismail Haniyeh, kiongozi wa kundi la wapiganaji wa Palestina la Hamas, akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya kukutana na Rais wa Lebanon Michel Aoun, katika ikulu ya rais, huko Baabda, mashariki mwa Beirut, Lebanon, Jumatatu, Juni. 28, 2021. Hamas ilisema Jumatano, Desemba 20. 2023, kiongozi wake mkuu, Ismail Haniyeh, amewasili Cairo kwa mazungumzo kuhusu vita huko Gaza. AP - Dalati Nohra
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo haya magumu ikiwa ni pamoja na kuachiwa upya kwa mateka yanaendelea kupitia nchi za upatanishi, Misri, Qatar na Marekani.

Bw. Haniyeh amesisitiza katika taarifa yake kwamba Hamas "haitakubali chochote isipokuwa kusitishwa kwa mapigano, kuondolewa kwa jeshi linalokalia kimabavu  Ukanda wa Gaza, kuondolewa kwa vizuizi vya kidhalimu na kutoa makazi salama kwa watu waliokimbia makazi yao.

Ameongeza kuwa watu waliokimbia makazi yao kutoka kaskazini mwa Ukanda wa Gaza wanapaswa kurejea katika makaazi yao, na ametoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa Hamas waliohukumiwa vifungo vya muda mrefu nchini Israel.

Siku ya Ijumaa Rais wa Marekani Joe Biden, kwa upande wake, aliomba "kusitishwa kwa muda kwa mapigano" ili kuruhusu kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas tangu Oktoba 7.

Jeshi la Israel linaendelea na operesheni zake za kijeshi huko Khan Younes, mji mkuu ulioko kusini mwa Ukanda wa Gaza uliowasilishwa kama ngome ya Hamas yenye sehemu ya chini ya ardhi iliyojaa mahandaki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.