Pata taarifa kuu

Israel: Shambulio la bunduki limesababisha vifo vya watu wasiopungua wawili kusini mwa nchi

Shambulio la bunduki kusini mwa Israel siku ya Ijumaa limesababisha vifo vya watu wasiopungua wawili na wanne kujeruhiwa. Mshambuliaji anaaminika kuwa Mpalestina kutoka Jerusalem. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anasema shambulio hili linaonyesha kuwa nchi nzima iko vitani.

Maafisa wa polisi wa Israeli wakipekua gari katika eneo la shambulio la bunduki karibu na manispaa ya Kiryat Malakhi kusini mwa nchi, Februari 16, 2024.
Maafisa wa polisi wa Israeli wakipekua gari katika eneo la shambulio la bunduki karibu na manispaa ya Kiryat Malakhi kusini mwa nchi, Februari 16, 2024. AP - Tsafrir Abayov
Matangazo ya kibiashara

 

Na mwandishi wetu maalum huko Jerusalem, Guilhem Delteil

Shambulio hilo lilitokea asubuhi, kando ya barabara yenye shughuli nyingi mashariki mwa mji wa Ashdodi. Mwanzoni mwa wikendi, watu kadhaa walikuwa wakisubiri kwenye kituo cha basi. Gari lilifika, mtu mmoja akashuka akiwa na bunduki. Aliwafyatulia risasi watu waliokuwepo katika kituo hicho.

Mshambuliaji huyo aliuawa na raia aliyekuwa akipita barabarani. Alikuwa Mpalestina na aliishi katika kambi ya wakimbizi huko Jerusalem. Hapo awali polisi ilizingira eneo hilo, ikitafuta watu walioweza kushirikiana naye lakini inabaini kwamba alitekeleza kitendo hicho peke yake.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amesema shambulio hili linaonyesh "kwamba nchi nzima iko vitani". Na "wauaji, ambao hawatoki Gaza tu, wanataka kutuua sisi sote," amesema.

Kwa upande wake, Waziri wa Usalama wa Umma anaona hii kama dtibitisho "kwamba silaha zinaokoa maisha." Nafasi ambayo ameitetea mara kadhaa tangu mashambulizi ya Hamas tarehe 7 Oktoba. Itamar Ben Gvir ambaye ni kutokea mrengo wa kulia, alitekeleza mpango uliolenga kusambaza silaha kwa raia na akaharakisha kushughulikia maombi ya vibali vya kumiliki silaha. Sera ambayo sasa anataka kuendeleza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.