Pata taarifa kuu

Canada kuwawekea vikwazo walowezi wa Ukingo wa Magharibi na viongozi wa Hamas

Canada itawawekea vikwazo walowezi wa Israel wanaochochea ghasia katika Ukingo wa Magharibi na kuwawekea vikwazo vipya viongozi wa Hamas, Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mélanie Joly, amesema siku ya Jumapili. Marekani ilichukua hatua kama hizo wiki iliyopita.

Mélanie Joly, Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, wakati wa ziara yake huko Kyiv, Ukraine, Februari 2, 2024.
Mélanie Joly, Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, wakati wa ziara yake huko Kyiv, Ukraine, Februari 2, 2024. © Evgeniy Maloletka / AP
Matangazo ya kibiashara

 

Katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Canada siku ya Jumapili, Mélanie Joly ametangaza kwamba baadhi ya walowezi “watawekewa vikwazo” na kwamba “pia tutaweka vikwazo vipya kwa viongozi wa Hamas.”

"Tunalifanyia kazi kwa bidii," amesema Mélanie Joly, akizungumza kutoka Ukraine. "Ninahakikisha kwamba nikiwa Ukraine, kazi inafanywa Ottawa na ninatazamia kutoa tangazo hivi karibuni." Siku ya Ijumaa Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau alisema kuwa anafikiria kuweka vikwazo kwa walowezi "wenye msimamo mkali" katika Ukingo wa Magharibi.

Tangu vita vya Mashariki ya Kati vya mwaka 1967, Israel imeukalia kwa mabavu Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, ambao Wapalestina wanataka kuuona kama moyo wa taifa huru. Israel ilijenga makazi ya Wayahudi katika Ukingo wa Magharibi kitendo ambacho nchi nyingi zinaona kuwa ni kinyume cha sheria. Israeli inapinga hili na inataja uhusiano wa kihistoria na kibiblia kwa nchi hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.