Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Saudi Arabia na Canada kurejesha uhusiano wa kidiplomasia

Saudi Arabia na Canada zitarejesha uhusiano wao wote wa kidiplomasia, Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia imetangaza Jumatano Mei 24, baada ya kutofautiana mwaka 2018 kuhusu haki za binadamu katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Mwanamfalme Mohammed bin Salman alijadiliana na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau ili kufikia hatua ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili.
Mwanamfalme Mohammed bin Salman alijadiliana na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau ili kufikia hatua ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili. AP - Leon Neal
Matangazo ya kibiashara

"Iliamuliwa kurejesha kiwango cha uhusiano wa kidiplomasia na Canada katika kiwango chake cha awali" baada ya majadiliano ya mwaka jana kati ya Mwanamfalme Mohammed bin Salman na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, wizara imesema katika taarifa.

Nchi hiyo ya kifalme ilikasirishwa mno baada ya waziri wa mambo ya nchi za nje wa Canada kuitolea wito iwaachie huru wanaharakati wa haki za binaadam.

Saudi Arabia  ilikosoa ujumbe huo kupitia ukurasa wa twitter ikisema unaingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo na kuwa unakiuka sheria za taifa hilo la Kifalme na pia mfumo wake wa kimahakama. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada Chrystia Freeland, katika ukurasa wake wa Twitter aliandika kuwa ana wasiwasi kuhusu kufungwa kwa wanawake hawa, hasa Samar Badawi.

Bi Badawi alikuwa akitoa wito wa kumalizika mfumo wa wanaume kuwasindikiza wanawake kila wanapokwenda.

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ilisema haiwezi kamwe kukubali kuingiliwa kwa masuala ya ndani ya nchi yao.

Mwanaharakati huyu anayetetea usawa wa kijinsia ni dada wa mwanablogu Raif Badawi, ambaye alifungwa nchini Saudi Arabia kwa miaka sita kwa kosa la kukosoa Uislam. Mke wake na watoto zake watatu wanaishi mjini Quebec, nchini Canada.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.