Pata taarifa kuu
USALAMA-DIPLOMASIA

Gaza: Israel na Islamic Jihad wafikia makubaliano ya kusitisha mapigano

Israel na kundi lenye silaha la Palestina, wamekubaliana kusitisha makabiliano, na kuleta matumaini ya kumaliza mapigano ya siku tatu ambayo yamekuwa yakiendelea katika ukanda wa Gaza na kusababisha vifo vya Wapalestina 44 wakiwemo watoto 15. 

Picha hii iliyopigwa kutoka mji wa Israel wa Ashkelon inaonyesha roketi zilizorushwa kutoka Ukanda wa Gaza mnamo Agosti 7, 2022.
Picha hii iliyopigwa kutoka mji wa Israel wa Ashkelon inaonyesha roketi zilizorushwa kutoka Ukanda wa Gaza mnamo Agosti 7, 2022. AFP - JACK GUEZ
Matangazo ya kibiashara

Makubaliano hayo yalifikiwa baada ya msaada wa Misri na tangu ulipoanza kutekelezwa saa tano na nusu usiku wa kuamkia leo, utulivu umeendelea kushuhudiwa. 

Hata hivyo, pande zote zimetishia kuendelea na mashambulio iwapo, upande mmoja utavunja makubaliano hayo. 

Uongozi wa Gaza umesema shughuli za kawaida zinatarajiwa kurejelewa tena hivi leo, ikiwa ni pamoja na wanafunzi kutarajiwa kuanza kurudi vyuoni. 

Rais wa Marekani Joe Biden, amepongeza hatua hii, huku akimshukuru rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi kwa kusaidia upatikanaji wa maelewano hayo, huku akitaka uchunguzi wa raia kuuawa. 

Ijumaa iliyopita, jeshi la Israel, lilishambulia eneo la Gaza na kuharibu majengo na kambi za wakimbizi, kwa kile walichosema, walikuwa wanawasaka viongozi wa kundi la kijihadi. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.