Pata taarifa kuu
UTURUKI-USHIRIKIANO

Diplomasia: Uturuki na Umoja wa Falme za Kiarabu kufufua uhusiano

Ankara na Abu Dhabi zinaelekea kuboresha mardhiano. Baada ya miaka mingi ya mvutano kati ya miji mikuu hii miwili, Mrithi wa kiti cha Ufalme wa Falme za Kiarabu Mohammed ben Zayed anatarajiwa kupokelewa Jumatano hii, Novemba 24 na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

Mwanamfalme wa Falme za Kiarabu Mohammed bin Zayed (kushoto) anatarajiwa kupokelewa Jumatano hii, Novemba 24 na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Mwanamfalme wa Falme za Kiarabu Mohammed bin Zayed (kushoto) anatarajiwa kupokelewa Jumatano hii, Novemba 24 na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. AFP - UMIT BEKTAS
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii ya Mohammed ben Zayed mjini Ankara, ambayo ni ya kwanza katika kipindi cha miaka kumi, inatarajia kurasimisha uhusiano wa Uturuki na Falme za Kiarabu ambao unatoka mbali. Kwa hakika, uhusiano kati ya Ankara na Abu Dhabi ulizorota taratibu tangu kuanza kwa "maandamano makubwa yaliyozuka katika nchi kadhaa za kiarabu", wakati Uturuki ilipoanza kuinuka kiuchumi na kudai kuwa ndio nchi enye nguvu katika katika ukanda huo na katika ulimwengu wa Kiislamu kwa ujumla.

Nchi hizo mbili zilijikuta katika pande zinazopingana wakati wa kupinduliwa kwa rais wa Misri Mohamed Morsi mwaka 2013, ambaye aliungwa mkono na Uturuki; kisha kuanzia mwaka 2017, na mgogoro kati ya nchi kadhaa za Ghuba na Qatar, mshirika mkuu wa Uturuki katika eneo lake.

Hivi majuzi, mgogoro wa Libya ulisababisha kuwepo malumbano zaidi kati ya Ankara na Abu Dhabi ambapo kuanzi mwaka 2019 Ankara iliunga mkono na kusaidia Serikali ya Umoja wa kitaifa iliyoko Tripoli. Ili kufanya mambo kuwa mabaya zaidi, maafisa wa Uturuki walishutumu Umoja wa Falme za Kiarabu kwa kufadhili jaribio la mapinduzi la Julai 15, 2016.

Ukaribu huu unatazamwa katika muktadha wa jumla zaidi ambao unaiona Uturuki ikijaribu kurekebisha uhusiano wake na mataifa mengine yenye nguvu za kikanda: Misri, Saudi Arabia, Israel. Kwa takriban mwaka mmoja, na kuingia madarakani kwa Joe Biden nchini Marekani, mgogoro mkubwa wa uchumi nchini Uturuki na Uturuki kuendele kutengwa katika mashindano ya nishati katika Bahari ya Mashariki, nchi ya Rais Recep Tayyip Erdogan inafuata sera ya kutegemeana.

Faida ya kiuchumi kwa Uturuki

Hii ni moja ya motisha kuu za Recep Tayyip Erdogan. Ankara inatarajia kuendeleza uhusiano wake wa kibiashara na Falme za Kiarabu, nchi tajiri. Kiasi cha biashara baina ya nchi hizi mbili kilikaribia dola bilioni 15 mwaka 2017, kabla ya kupunguzwa kwa nusu katika miaka iliyofuata, dhidi ya hali ya mzozo kati ya Qatar. Hasa, kiasi cha mauzo ya nje ya Uturuki kiligawanywa na tatu.

Rais Erdogan pia amesisitiza hadharani na mara kwa mara katika miezi ya hivi karibuni juu ya uwekezaji ambao Umoja wa Falme za Kiarabu unaweza kufanya nchini Uturuki. Abu Dhabi inasemekana kupendezwa sana na tasnia ya ulinzi ya Uturuki, ambayo imekuwa na nguvu sana katika miaka ya hivi karibuni. Uwekezaji unaotarajiwa na Uturuki unafikia mabilioni, hata makumi ya mabilioni ya dola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.