Pata taarifa kuu
SYRIA-IS

IS yatangaza kifo cha msemaji wake Al Adnani

Msemaji wa kundi la Islamic State (IS), Abu Mohamed al Adnani, ambaye alitoa wito mwaka 2014 wa kuua raia wa Ufaransa "kwa njia zote", ameuawa katika mkoa wa Aleppo, shirika la habari la IS la Amaq limearifu.

Abu Mohammed al-Adnani, katika video iliyorushwa na kundi la Islamic State, tarehe 8 Julai 2012.
Abu Mohammed al-Adnani, katika video iliyorushwa na kundi la Islamic State, tarehe 8 Julai 2012. HO / YOUTUBE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Amaq imesema katika taarifa iliyosambazwa kwa wafuasi wa asasi za kijihadi kwamba msemaji wake ameuawa "wakati alipokua akisimamia shughuli za kurejesha nyuma kampeni za kijeshi dhidi ya mkoa wa Aleppo."

Kundi la Islamic State bado linadhibiti maeneo kadhaa katika mkoa wla mashariki wa Aleppo lakini si katika mji wenyewe, ambapo waasi wa Syria wanaendelea na mapigano makali dhidi ya vikosi vya Serikali ya Syria na washirika wao.

Amaq hajasema lini Abu Mohamed al Adnani aliuawa. Tangazo la kuuawa kwa msemaji wa kundi la Islamic State liliandikwa tarehe 29 Agosti lakini halijataja tarehe ya kifo chake.

Kundi hili la wanajihadi hivi karibuni lilipoteza vitu na wapiganaji wake kadhaa katika jimbo la Aleppo, katika mapigano nawaasi wa Syria wa kundi la FDS, linajumuisha wapiganaji wa Kiarabu na Wakurdi wanaoungwa mkono na Marekani, na hivi karibuni dhidi ya waasi wanaoungwamkono na Uturuki.

Abu Mohamed al Adnani , mzaliwa wa mji wa Idlib kaskazini magharibi mwa Syria, alikuwa kwa miaka miwili afisa mkuu anayehusika na kueneza propaganda ya kundi la Islamic State.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.