Pata taarifa kuu
SYRIA-IS-UGAIDI

Kundi la IS latangaza kifo cha Omar, raia wa Chechenia

Omar al-Chichani (Omar Chechen), mmoja wa makamanda maarufu wa kundi la Islamic State aliuawa nchini Iraq. Shirika la habari la Qama, lenye mahusiano na kundi la Islamic Satte limearifu, lakini halikusema lini aliuawa.

Picha ya Omar al-Shishani iliyotolewa kwenye tovuti ya kijihadi, Juni 29, 2014.
Picha ya Omar al-Shishani iliyotolewa kwenye tovuti ya kijihadi, Juni 29, 2014. AFP PHOTO / HO / Al-Itisam Media
Matangazo ya kibiashara

Kifo chake "kama ni kweli" kilikua kimeshatangaza. Kama kifo hiki kitakua kimeshibitishwa, ni pigo jingine kubwa kwa kundi la IS, kwani Omar al-Chichani alikuwa kiungo muhimu na mtu maarufu katika kundi hili.

Omar Chechen alikuwa mtu muhimu kwa kundi la Islamic State.
Omar al-Chichani alizaliwa mwaka 1986 kwa mama Mkristo na baba Muislamu, katika mji mdogo wa Caucasus, kaskazini mwa Georgia. Eneo hili linachukuliwa na baadhi ya watu, hasa Warusi kama kituo cha ugaidi wa Kiislam.

Tarkhan Batirashvili, jina lake halisi, alihudumu akiwa na umri wa miaka 21 katika jeshi la Gergia. alishiriki katika vita kati vya Georgia na Urusi mwaka 2008. Lakini mwaka 2010, alikamatwa na kutiwa hatiani kwa kumiliki silaha kinyume cha sheria. Hata hivyo baada ya kubainika kuwa ana maradhi ya kifua kikuu, Omar Al-Chichani aliachiliwa huru miezi kumi na sita baadaye. Tangu wakati huo alitoweka na kuonekana tena mwaka 2013 nchini Syria, katika la kundi Islamic State, akijulikana kwa jina la Abu Omar al-Chichani.

Kutokana na ujuzi wake wa kimkakati, aliteuliwa haraka kama kiongozi wa harakati za kundi la Islamic State kaskazini mwa Syria. Kisha akawa mmoja wa viongozi wa kijeshi wa kundi la IS. Ushujaa wa Omar al-Chichani ulitumiwa sana kwa propaganda za kundi la Islamic State ili kuvutia vijana wa Caucasus kujiunga na kundi hilo.

Mwezi Machi, Marekani ilitangaza kuwa kiungo huyo wa ugaidialiuawa katika shambulio la anga. Lakini shirika la Haki za Binadamu, lenye makao yake nchini Uingereza, ambalo lina mtandao mkubwa nchini Syria lilikanusha taarifa hiyo. Wakati huu, kundi la Islamic State limeamua kutangaza kuwa kiungo wake muhimu hayupo tena duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.