Pata taarifa kuu
UFARANSA

Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa yalaani kitendo cha waziri wa Ufaransa kufananishwa na nyani

Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa UN, hii leo imetoa tamko kulaani vikali baadhi ya wanasiasa na wananchi wa nchini Ufaransa, kumdhalilisha waziri wa sheria nchini humo mwenye asili ya watu weusi na kumfananisha na nyani. 

Waziri wa Sheria wa Ufaransa, Christiane Taubira
Waziri wa Sheria wa Ufaransa, Christiane Taubira Reuters
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na wanahabari, msemaji wa tume ya haki za binadamu ya umoja huo, Rupert Colville, amesema kuwa tume yake inalaani vikali matamshi ya baadhi ya wanasiasa wa Ufaransa hivi karibuni kumfananisha na nyani waziri wa sheria wa Ufaransa mwenye asili ya watu weusi, Christiane Taubira.

Colville, ameongeza kuwa kitendo kilichoshuhudiwa nchini Ufaransa, hakikubaliki kwenye jumuiya ya kimataifa na kinaonyesha jinsi gani vitendo vya ubaguzi wa rangi vinazidi kuongezeka hali inayowafanya wageni wengi kwenye mataifa ya ulaya wenye asili ya watu weusi kuhofia maisha yao.

Juma hili gazeti moja nchini Ufaransa la kila wiki lilichapisha picha ya waziri Toubira kwenye ukurasa wake wa mbele huku likimchora uso uliofanana na nyani likiwa na kichwa cha habari kinachosema hatimaye nyani amepata ndizi yake.

Kwenye utetezi wake wakuu wa gazeti hilo wamekataa kuomba radhi wakisema neno hilo kwa jamii ya watu wa Ufaransa linamaana mbili moja ikiwa ni mtu aliyejawa na furaha jambo ambalo tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa UN inakataa.

Waziri Toubira amejikuta matatani na wananchi wa Ufaransa kufuatia hatua yake ya kupendekeza na kisha kupitishwa kwa muswada unaotambua ndoa za watu wa jinsia moja ambao uliungwa mkono na wabunge nchini humo.

Kwenye maandamano yao kupinga kupitishwa kwa sheria hiyo, waandamanaji walikuwa wamebeba ndizi na picha za kiongozi huyo akifananishwa na nyani wakimtaka aende akaishi msituni na sii kwenye jamii ya watu waliostaarabika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.