Pata taarifa kuu
ZANZIBAR-TANZANIA

Mwanasiasa mkongwe wa Zanzibar Maalim Seif Sheriff Hamad afariki dunia

Mwanasiasa mkongwe na Makamu wa Kwanza wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Sheriff Hamad amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 77.

Mwanasiasa mkongwe na Makamu wa Kwanza wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Sheriff Hamad, siku za uhai wake
Mwanasiasa mkongwe na Makamu wa Kwanza wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Sheriff Hamad, siku za uhai wake ACT WAZALENDO ZANZIBAR:twitter.com
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi, kupitia hotuba kwa Wazanzibari, amesema Seif amefariki dunia akiwa katika Taasisi ya Magonjwa ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.

Mwezi Januari, chama chake cha ACT Wazalendo kilitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwamba Makamu huyo wa kwanza wa rais na wake na watu ndani ya familia yake walipata maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Katika uhai wake, mwanasiasa huyo mkongwe ambaye pia aliwahi kuhudumu kwa muda mrefu kama Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF na baadaye kuondoka na kuhamia chama cha ACT Wazalendo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, na kuwa Mwenyekiti wake, anaelezwa kama mwanasiasa alieypigania haki za Wazanzibari.

Safari yake kutaka kuwa rais wa Zanzibar, ilianza mwaka 1995 baada ya Tanzania kui ngia kwenye mfumo wa vyama vingi, na aliwania nyadhifa hiuyo kupitai chama cha CUF kipindi chote cha uchaguzi mpaka 2015 na kushindwa na mgomùbea wa chama tawala CCM, lakjini nyakati hizo zote, alidai kuibiwa kura. Uchaguzi wa mwaka 2020 aliwania pia urais kupitia chama cha ACT Wazalendo.

Amefariki dunia, baada ya kuwa madarakani kama Makamu wa kwanza wa rais kwa zaidi ya siku 100 tangu alipoamua kuungana na rais Hussein Ali Mwinyi, kuongoza katika serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.