Pata taarifa kuu
RWANDA-UFARANSA-HAKI

Wakili wa Aloys Ntiwiragabo: Habari za Gazeti la Mediapart ni 'za uwongo'

Baada ya Gazeti la Médiapart kuchapisha habari kuhusu kuhusika kwa mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi wa kijeshi nchini Rwanda, Aloys Ntiwiragabo, katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, mwanasheria wake Benjamin Chouai amebaini kwamba mteja wake yuko tayari kujibu maswali yoyote ya mahakama ya Ufaransa.

Waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR, kilomita 150 kaskazini mashariki mwa Goma, mwaka 2009.
Waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR, kilomita 150 kaskazini mashariki mwa Goma, mwaka 2009. AFP/ Lionel Healing
Matangazo ya kibiashara

Kauli hi inakuja siku chache baada ya ofisi ya mashtaka dhidi ya ugaidi nchini Ufaransa kutangaza kufunguliwa kwa uchunguzi wa awali kuhusu uhalifu dhidi ya binadamu dhidi ya afisa huyo wa zamani wa Rwanda.

Hata hivyo wakili Benjamin Chouai amekumbusha kwamba mteja wake, Aloys Ntiwiragabo, hivi leo hatafutwi na mtu yeyote, wala ICTR, wala mahakama ya Rwanda ... na hasa kwamba hajawahi kujificha.

Wakili wa Aloys Ntiwiragabo ameliomba Gazeti la Médiapart kumpa mteja wake nafasi ya kujibu dhidi ya madai hayo na kutishia kufungulia mashitaka vyombo vingine vya habari vya Ufaransa.

"Mteja wetu anakanusha habari iliyochapishwa na tovuti ya Mediapart," wakili Chouai amewema katika mahojiano na Sonia Rolley.

Ofisi ya mashtaka inabaini kuwa hadi leo hakuna malalamiko yoyote au hati ya waranti dhidi ya afisa huyo mwandamizi wa zamani wa Rwanda, iwe nchini Ufaransa, Rwanda au kutoka polisi ya kimataifa, Interpol.

Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ya Rwanda (ICTR) ilitoa waranti wa kukamatwa dhidi yake mnamo mwaka 1998 na 2002, kisha kufutwa miaka kadhaa iliyopita. Katika mashtaka ya ICTR, Aloys Ntiwiragabo anatajwa kama sehemu ya kikundi cha maafisa ambao kati ya mwaka 1990 na 1994 "walikubaliana kupanga mpango kwa nia ya kuwaangamiza raia kutoka jamii ya Watutsi na wanasiasa wa upinzani na hivyo kubaki madarakani ”. Iilidaiwa pia kuwa kulikuwa kukitolewa kila mara orodha ya Watutsi na wapinzani ili "kuangalmizwa". Lakini waranti zote hizo za kukamatwa zilifutwa miaka kadhaa iliyopita.

Nchini Ufaransa, kulingana na upande wa mashtaka, kutajwa tu kwa jina lake kulianzia mwaka 2011 wakati mahakma ya kupambana na ugaidi ya Ufaransa ilipotaka kumsikiliza kama shahidi katika muktadha wa utaratibu uliolenga mmoja wa wasaidizi wake. Wakati huo, viongozi wa Rwanda walidai kwamba Aloys Ntiwiragabo alikuwa mafichoni katika moja ya nchi za Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.