Pata taarifa kuu

Kesi ya Habyarimana: Mashitaka dhidi ya washirika wa karibu wa Paul Kagame yafutwa

Mahakama ya Rufaa ya Paris imethibitisha uamuzi uliotolewa na majaji mwishoni mwa mwaka wa 2018 wa kufuta kesi dhidi ya washirika saba wa Rais wa Rwanda Paul Kagame, ambao walishtakiwa kwa kudungua ndege ya rais Habyarimana.

Rais wa zamani wa Rwanda Juvénal Habyarimana (hapa ilikuwa mwaka 1982).
Rais wa zamani wa Rwanda Juvénal Habyarimana (hapa ilikuwa mwaka 1982). AFP
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo linachukuliwa kuwa ndio chanzo cha mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994 nchini Rwanda.

Mahakama y Rufaa haijaelezea sababu zake kwa kuchukuwa uamuzi huu. Upande wa utetezi unasema umefurahishwa na uamuzi huo, hata kama uamuzi huu haufunge kabisa faili hii. Vyama vya kiraia tayari vimetangaza kukata rufaa.

Mwaka 2018 Mahakama ya mwanzo nchini humo ilifutilia mbali kesi hiyo, ambayo ilianzishwa tangu miaka 20 iliyopita.

Kesi hii ya "mauaji na kula njama kwa ushirikiano kundi la kigaidi" ilifunguliwa nchini Ufaransa mnamo mwaka 1998, kufuatia malalamiko yaliyotolewa na familia za marubani kutoka Ufaransa, waliokuwa wakiendesha ndege hiyo ya rais Habyarimana.

Majaji wawili wa Ufaransa wa kitengo kinachopambana dhidi ya ugaidi waliokuwa wakishughulikia kesi hiyo waliamua kuachana nayo Desemba 21, 2018, "baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha", kwa mujibu wa majaji hao ambao pia walibaini kuwepo na "hoja zinazopingana na ambazo hazikuchunguzwa" kuhusiana na ushahidi uliokusanywa.

Mawakili wa upande wa mashitaka wanataka hasa kwamba mahakama ya Ufaransa ipate ripoti ya siri ya mwaka 2003 kutoka kwa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai iliyoundwa kwa ajali ya Rwanda.

Rais Juvenal Habyarimana aliuawa na mwenzake wa Burundi Cyprien Ntaryamira katika shambulio dhidi ya ndege yao wakati ndege hiyo ilipokuwa ikijaribu kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa aw Kanombe jijini Kigali ikitokea nchini Tanzania katika mazungumzo ya kusaka amani nchini Rwanda, Aprili 6, 1994.

Baada ya tukio hilo, machafuko yalizuka, na watu zaidi ya Laki nane, wengi wao kutoka jamii ya Watutsi waliuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.